Fresha Kinasa. Mara.
NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii Dunstan Kitandula amesaema kuwa, serikali inalenga ifikapo mwaka 2030 kaya Mil. 15 ziwe zinatumia Kilimo mseto hapa nchini.
Kitandula ameyasema hayo Novemba 14, 2023, wakati akifungua maonesho ya tisa ya Kilimo mseto yanayofanyika katika Kata ya Bweri Manispaa ya Musoma kuanzia Novemba 14, hadi Novemba 16, 2024. Ambapo yanawaleta pamoja wadau mbalimbali wa Kilimo mseto kutoka serikalini, sekta binafsi na wananchi kwa ujumla.
Amesaema kuwa, Wadau wa mazingira na Kilimo mseto wanalojukumu la kushirikiana katika utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa Kilimo mseto uliozinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania machi 2024, huko Same Mkoani Kilimanjaro.
Ambapo, Wizara ya Maliasili na Utalii ndio msimamizi wa mkakati huo, unaolenga kuhamasisha Kilimo mseto katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, lishe bora pamoja na kukuza kipato. Huku akiweka wazi kwamba, serikali ina mpango wa kutafsiri mkakati huo katika lugha ya kiswahili ili kuwafikia wadau wengi.
Pia amesistiza kuanzishwa kwa jukwaa la Kilimo mseto litakaloratibu utekelezaji wa mkakati huo pamoja na shughuli na jitihada za wadau mbalimbali hapa nchini. Huku pia akiagiza kuanzishwa na kuendelezwa kwa bustani ya miti yenye kuendana na Kilimo mseto.
Ameongeza kuwa, sekta binafsi zinalojukumu la kuwekeza kwenye kuongeza thamani na kujenga masoko kwa mazao yanayotokana na Kilimo mseto. Na kuonbgeza miradi ya biashara ya kaboni kwenye maeneo ya Kilimo mseto.
"Mifumo endelevu ya Chakula ndio itahakikisha usalama wa Chakula nchini, na usalama wa Chakula unajengwa na misingi minne ambayo ni upatikanaji wa Chakula, ufikikaji wa Chakula, utumiaji wa chakula na uendelevu wa Chakula."amesema Naibu Waziri Kitandula.
Aidha, Kitandula amelishukuru Shirika la Vi -Agroforestry kwa kuendelea kushirikiana na Serikali na wadau mbalimbali wa Kilimo mseto na uhifadhi wa mazingira. Kwani Jambo hilo lina mchango mkubwa Sana katika uendelevu wa Chakula, kuboresha mazingira hapa nchini.
Kwa upande wake Katinka Sofia Palmgeren kutoka Shirika la Vi-Agroforestry amesema kuwa maonesho hayo ya siku tatu yanatarajia kuwaunganisha washiriki 5000 wakiwemo wakulima wadogo, Maafisa wa serikali, Wawakilishi wa sekta binafsi, na Wajumbe kutoka Asasi za Kiraia.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi, Mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka, amesema kuwa, maonesaho hayo yameleta mabadiliko kwa Wakazi wa Mara katika kufanya Kilimo bora kwa kipindi ambacho yamekuwa yakifanyika.
"Niwaombe Wananchi, mje mpate elimu na ujuzi kwa Kilimo bora hii ni fursa kwa Wananchi wa Mara katika kuleta Mapinduzi katika Kilimo chenye tija."amesema Chikoka.
![]() |



