Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongoza Waombolezaji kuaga mwili wa aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Marehemu Lawrence Nyasebwa Mafuru katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaa, leo tarehe 14 Novemba, 2024.
Katika salamu zake za pole kwa familia na Watanzania Rais Samia amesema kifo cha Mafuru kimeacha pengo kubwa kwa taifa hasa kutokana na mchango wake mkubwa wa kujitolea kwa taifa lake.
Kwa sababu hiyo Mh Rais Dkt Samia amesema Laurence alikuwa zawadi kwa taifa lake na kwamba alikuwa ni mmoja wa mashujaa wa Tanzania.
Amesema ushujaa unaweza kujitokeza kwa namna mbali ikiwemo kufanya kazi kwa bidii na kujitoa kwa taifa lako bila kuchoka,hivyo Mafuru anastahili sifa hiyo.
Mh Rais Samia amesema Lawrence amekuwa na mchango mkubwa katika sekta binafsi na sekta ya umma na ameacha alama ambayo haitafutika hasa katika mageuzi makubwa ya uendeshaji wa mashirika ya umma aliyofanya akiwa msajili wa hazina.
Amesema kutoka na uchapa kazi wake,sifa zake za ubunifu na ueledi baada ya tu kuwa Rais wa nchi aliweza kumteua kuwa kamishina wa sera wa ilikuwa wizara ya fedha na mipango,badae alimteua kuwa naibu katibu mkuu wizara ya fedha anashughulikia uchumi na sera.
Rais Samia amesema uchapakazi na ubunifu wa Lawrence ulimfanya pia amteue kuwa katibu mtendaji wa tume ya mipango baada ya tume hiyi kuanzishwa nafasi aliyokuwa nayo hati Mauti yamemkuta.
Awali waziri mkuu Kassim Majaliwa,akizungumza wakati wa kumkaribisha Rais Samia,ametoa Pole kwa Rais kuondokewa na mtumishi huyo,famia na Watanzania huku akisema uchapakazi wa Mafuru unapaswa kuigwa na kila Mtanzania kwa maendeleo ya taifa letu.
Katika tukio hilo mbali na familia ya Mafuru viongozi mbalimbali wa sekta binafsi na sekta ya umma wameudhuria,wakiwemo wawakilishi kutoka nje ya nchi ambao wametoa salamu zao na kusema taifa limepoteza mtu muhimu.
Mwili wa Marehemu Lawrence Mafuru ambaye amezaliwa mwaka 1972 anayetarajiwa kuzikwa kesho Novemba 15 jijini Dar es Salaam,ameacha mke na watoto pamoja na wazazi Baba na Mama.








.jpg)
















.jpg)



