Sister Nyakuba amesema kuwa ametoa vifaa hivyo ili viweze kutumiwa kwenye utendaji kazi wa chama hicho.
Vifaa hivyo vimepokelewa na Katibu wa CCM wilaya Musoma Burhan Ruta ambaye amesema chama hicho kinatoa shukurani za dhati kwa msaada huo ambao utasaidia katika maandalizi ya shughuli za uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Ruta amesema kwamba chama hicho kinaendelea kuthamini mchango wa Mjumbe huyo wa kamati tendaji ya UWT Mkoa wa Mara.
Mjumbe wa Kamati tendaji ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)mkoa wa Mara Sister Yohana Nyakuba pia Katibu wa CCM kata ya Mwisenge (CCM) Ibambai ,Ream na kalamu kwa ajili ya kufanikisha utendaji wa kazi ikiwemo maandalizi ya shughuli za uchaguzi Serikali za Mitaa.


