Akizungumza wakati wa kutembelea bandari hiyo,Juliana amesema kuwa uwekezaji huo utachochea Maendeleo ya kiuchumi katika mkoa wa Mtwara na Taifa kwa ujumla.
Aidha Mhe. Juliana Masaburi amempongeza Meneja wa Bandari ya Mtwara, Ndugu Fernand Nyati kwa kusimamia vyema Bandari ya Mtwara na kujipanga vyema kwa maandalizi ya kusafirisha Korosho kwa kupokea Meli zaidi ya 3 zenye makasha ya kusafirisha Korosho hizo.
Katika ziara hiyo,Mhe.Juliana aliambatana baraza la umoja wa vijana wa chama chamapinduzi (UVCCM)Mkoa Mtwara ambapo Mwenyekiti wa umoja huo,Komredi Abuu Athumani amesema kuwa wameamua kumleta Mgeni, Mhe. Juliana Masaburi kutembelea Bandari ya Mtwara ili aone uwekezaji wa Serikali na Baraza la Vijana lipate la kujifunza kupitia Bandari hiyo.
Mbunge Juliana Didas Masaburi ameenda Mtwara kwa ajili ya kushiriki Kikao cha Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mtwara kilichofanyika 05 Oktoba, 2024 katika Ukumbi wa Bandari ya Mtwara
Aidha, Mhe. Juliana Masaburi akiwa katika Kikao cha Baraza la UVCCM Mkoa wa Mtwara ametoa kiasi cha shilingi Milioni Moja (1,000,000) na Matofali 1000 kwaajili ya ujenzi wa nyumba ya Katibu wa UVCCM Mkoa wa Mtwara na pia, amegawa vyeti vya pongezi kwa wadau wa UVCCM Mkoa wa Mtwara.