Watakaobainika Kugombea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Bila Kuwa na Sifa Kagera Kuchukuliwa Hatua

GEORGE MARATO TV
0

 


Na Angela Sebastian-Bukoba 

MKUU wa mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwassa amewatahadharisha watu wasio na sifa za kugombea katika uchaguzi wa Serikali za mitaa hususani wahamiaji haramu, kutodhubutu kuchukua fomu na wakibainika  watachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria 

Hajat Mwassa amebainisha  wakati akiongea na vyombo mbalimbali vya habari ofisini kwakwe wakati akitoa taarifa kwa Umma juu ya uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika nchi nzima  Novemba 27 mwaka huu.

"Sisi mkoa wetu uko mpakani tunajua kabisa kuwa wapo watu ambao wameingia hapa nchini na wengine wamebaki bila kutoka hivyo wanaishi kinyume cha sheria na taratibu za nchi na  wangependa kuwa viongozi na wengine wanatumia mbinu mbalimbali ikwemo rushwa ili wachaguliwe kuwa viongozi wakijaribu kugombea tutawachukuli za kisheria"

Pia amewatahadharisha wananchi wa Kagera kutochagua watu ambao si watanzania kwani uchaguzi huu ni kwa ajili ya watanzania pekee hivyo mwenye haki ya kuchagua na kuchaguliwa kwa mujibu wa katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ni mtanzania tusiweke mamluki kwenye nchi yetu tusilete hatari na kusababisha hatari ndani ya nchi yetu.

Amesema mkoa wa Kagera unakadiriwa kuwa na watu wenye umri wa miaka 18 na kuendelea wapatao milioni 1.5 wanawake wakiwa laki 7.5 na wanaume laki 8.2 ambapo vipo vituo vya uandikishaji wapiga kura 3,833 hivyo amewashauri wananchi kujitokeza kujiandikisha ili wapate fursa ya kutumia haki yao ya msingi na kikatiba ya kupiga kura na kugombea nafasi za uongozi.

Amesema uandikishaji utaanza Oktoba 11 hadi 20 

mwaka huu huku zoezi la kuchukua na kurejesha form likianza Novemba mosi hadi saba mwaka huu ambapo amewataka wagombea wote wa mkoa huo wa vyama vyote kufanya kampeni za kistaarabu na zenye staha kwa kunadi sera zao ili kuwapa wananchi nafasi ya kuchambua na kuchagua  viongozi bora.

Amesema wale ambao wanachangamoto ya kutembea utawekwa utaratibu mzuri zaidi ata kama ni viti mwendo waweze kufikishwa kwenye vituo wapige kura.





Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top