Ivona Bajumuzi Awashauri Wanawake Wajasiliamali Kagera Kusaidiana

GEORGE MARATO TV
0

 


Na Angela Sebastian- Bukoba

MWENYEKITI wa chama cha wanawake wajasiriamali mkoani Kagera (TWCC)  mwalimu Ivona Bajumuzi amewashauriwa wanawake wajasiriamali kutafuta namna ya kuwakwamua wenzao kwa kuwapa elimu ambao bado wanashindwa kuondokana na utegemezi kwa wenza wao ili waweze kujiongezea kipato kupitia ujasiriamali.

Bajumuzi ametoa ushauri huo wakati akiongea na baadhi ya wanawake wajasiriamali wa Manispaa ya Bukoba waliopata mafunzo ya ujasiriamali yaliyoandaliwa na kampuni ya Stain Group na kufanyika katika ukumbi wa mtakatifu Theresa Bukoba mjini.

"Kwasasa hakuna haja ya wanawake kuendelea kuwa tegemezi kwa wenza wao au mtu yoyote hivyo wale ambao tayari wameshapiga hatua za kibiashara wawasaidie wengine kuwapa mbinu za kufanya ujasiriamali kwa kuwapa mawazo,umuhimu na faida za kufanya ujasiriamali ili nao waweze kujikwamua na wimbi la umaskini "alisema Bajumuzi. 

Amesema wanawake wengi wanashindwa kufanya ujasiriamali na kisimama wenyewe kutokana na changamoto za kwamba nitapata wapi mtaji, masoko ya vile atakavyozalisha, uwezeshwaji duni wa kielimu,changamoto za familia ikiwemo malezi, msongo wa mawazo na kipato duni.

Aidha Bajumuzi aliwataka wanawake kutobagua kazi kwa mfano mtu kutembeza dagaa kwenye beseni anaona kama amedhalilika lakini watambue kuwa hakuna tajiri yoyote aliyeanza na mtaji mkubwa bali wote walianza kidogokidogo na sasa ni wafanyabiashara wakubwa.

"Napongeza Serikali yetu kwa kuruhusu yafanyike mafunzo kama haya kutoka kwa wadau mbalimbali pia napongeza kampuni ya Stain kutoa elimu hii kwa

wanawake kwasababu wakiwezeshwa kupata elimu kama hii ya ujasiriamali wataondokana na hari ya kubaki tegemezi na kufanya ujasiriamali endelevu utakao watoa sehemu moja kwenda nyingine "alisema Bajumuzi

Kwa upande wake meneja wa Stain Media mkoa wa Kagera Exavery Shumbusho alisema kuwa mafunzo hayo ni endelevu katika Halmashauri zote nane za mkoa huo  hivyo wamelenga wanawake kwasababu waliowengi mara nyingi wanakuwa hawajiamini lakini wakipata mafunzo kama haya itawaongezea kuiutuma na kuiga mfano wa viongozi wakubwa kama vile Rais Samia Suluhu na wengine ambao wameweza kusimama na kufanya makubwa.

"Mafunzo haya yatasaidia kizazi cha sasa na kijacho cha watu wanaojiamini wanaojiweza kiuchumi na kuacha kuwa tegemezi"alisema Shumbusho 

Naye Mkurugenzi wa Stain Group Mayamba Mbilinyi aliwashauri wanawake hao kuendelea kuchangamkia fursa za elimu kama hizo huku akiwataka vijana kujiandaa kupata mafunzo ambayo yanatarajia kufanyika mkoa mzima muda si mrefu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top