Na Angela Sebastian-Bukoba
Mkuu wa mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwassa ametoa wito kwa wananchi wa mkoa huo kutumia fursa inayotolewa na Serikali ambayo ni hupatikanaji wa elimu kwa watu wazima na nje ya mfumo rasmi ili kujiendeleza na kupata kujua stadi za maisha zitakazowasaidia kuwepo na jamii ya watu walioelimika.
Katika taarifa iliyosomwa na Afisa elimu wa mkoa wa Kagera Michael Ligola akisoma risala ya kufunga maadhimisho ya kilele cha wiki ya elimu ya watu wazima kwa niaba mkuu wa mkoa wa Kagera Hajat Mwassa jana ,katika viwanja vya mji mdogo wa Kayanga Wilaya Karagwe ambapo alisema kuwa maadhimisho hayo ni utekelezaji wa sera ya elimu.
"Sera hiyo iliaksi malengo yaliyoko katika dira ya Taifa ya maendeleo ya mwaka 1925 na malengo endelevu ya dunia (SDG) ambapo moja ya lengo la dira ya mwaka 2025 ni kuhakikisha kuwa Tanzania ifikapo 2025 inakuwa na watu waliosoma na jamii iliyoelimika sambamba malengo endelevu ya dunia yanayosema elimu kwa wote ifikapo 2030"ameleza
Anasema Serikali ya mkoa wa Kagera imedhamilia kutimiza azima ya kuwa na watu walioelimika kwa kushamilisha kauli mbiu ya wiki ya elimu ya watu wazima mwaka huu inayosema ujumuishi katika elimu bila ukomo kwa ujuzi,ustaimilivu amani na Maendeleo.
Anasema eneo la elimu ya watu wazima na nje ya mfumo rasmi inajumuisha makundi matano ambayo ni MEMKWA,MESKWA,MUKEJASEQUIP na Elimu ya ufundi haya yote yanafanyika ili kuhakikisha wananchi wanakuwa na elimu yenye ujuzi na maarifa ya kuwawezesha kuwa, sehemu ya mfumo wa dunia ambao umejikita katika ufahamu,maharifa na teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA).
Aidha Mwassa ameitaka idara ya elimu mkoa huo kuona fahari ya uwepo wa idadi nyingi ya vyuo na vituo vinavyotoa elimu ya watu wazima hivyo vitumike kuondoa kabisa idadi ya watu wasiojua kusoma,kuandika na kuhesabu kutoka asilimia 3.3 kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.
Naye Afisa elimu ya watu wazima na nje ya mfumo rasmi na elimu maalum mkoa wa Kagera Fortunatus Kahwa amesema idara ya elimu na wadau wanaendelea kushirikiana kuhakikisha changamoto ya uwepo watu wazima 4184 mkoni humo kuanzia miaka 19 na kuendelea wasiojua kusoma,kuandika na kuhesabu inafanyiwa kazi .





Comments
Post a Comment