Waziri mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) aende mara moja Wilaya ya Temeke na kutembelea viwanda vinavyolalimikiwa kutiririsha maji kwenye makazi ya watu na barabara.
Mh Waziri mkuu,ametoa agizo hilo leo jumamosi Oktoba 05,2024 wakati akihutubia wa Temeke eneo la Mbagala Kizuiani siku ya kwanza ya ziara yake mkoani Dar es salaam.
Amesema amepata malalamiko mengi ya wananchi kuhusu baadhi ya viwanda kutiririsha maji kwenda kwenye makazi ya watu na maeneo yasiyostahili hivyo kumtaka Mkurugenzi huyo wa NEMC kufika wilayani Temeke jumatatu ya Oktoba 07 ili aweze kutembelea maeneo hayo na kuchukua hatua za kutatua kero hiyo kwa wananchi.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kutoa fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye sekta zote ikiwemo Afya, Maji, Elimu na Miundombinu ya Barabara.
Amesema kuwa Serikali ipo imara na imedhamiria kuendelea kuwatumikia watanzania wote. “Niwahakikishie kuwa Rais wetu Dkt. Samia yupo imara na anaupendo kwa Watanzania, dhamira, mipango na mienendo yake ya utawala ipo safi”.
Kuhusu Nishati safi ya kupikia mh waziri mkuu,amewataka Watanzania kumuunga mkono Rais Samia katika kampeni yake hiyo inayolenga kuketa mabadiliko makubwa katika kupambana na matumizi ya kuni na mkaa hapa nchini.
Amesema kuwa katika kuhakikisha juhudi hizo za Mh Rais Samia zinafanikiwa tayari Serikali imeagiza ifikapo mwezi Desemba mwaka huu taasisi zote zenye watu wanaotukia kuni na mkaa zikiwemo ya elimu,majeshi na afya kusitisha matukizi hayo badala yake zitumie nishati ya Gesi na Umeme.
Waziri mkuu pia amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Ndg. Jomaary Satura kuhakikisha anatumia fedha za mapato ya ndani kuweka taa za barabarani katika maeneo yote yenye uhitaji
Pamoja na mambo mengine, Mheshimiwa Majaliwa amekagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya ghorofa sita ya Mbagala Rangi tatu ambayo ujenzi wake unatarajiwa kugharimu shilingi bilioni 10.85 na itasaidia kulaza wagonjwa 165.
Ujenzi wa hospitali hiyo utasaidia kuboresha huduma za afya zikiwemo za kibingwa, kutoa huduma ya upasuaji mkubwa, huduma za dharura, kupunguza msongamano uliopo kwa sasa, kuongeza wigo wa utoaji huduma kwa
wananchi, kupunguza rufaa zisizo na ulazima na kuhudumia wananchi wa Mbagala na maeneo ya jirani.
Pia, Mheshimiwa Majaliwa alikagua Ujenzi, Upanuzi na Ukarabati wa Daraja na Barabara ya Mivinjeni na Bandari One jijini Dar es Salaam






.jpg)

.jpg)

Comments
Post a Comment