Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa onyo kali kwa wale wote wajihusha na vitendo vya kukatisha masomo watoto kwa kike na kusema kuwa serikali ya awamu ya sita imeweka mikakati mbalimbali ya kumlinda mtoto wa kike, ikiwa ni pamoja na kutunga sheria kali dhidi ya watu hao.
Waziri mkuu ametoa kauli hiyo Oktoba 05,2024 wilayani Temeke mkoani Dar es Salaam baada ya kuzindua jengo la bweni kwa ajili ya wanafunzi wa kike likiwemo jengo bwalo la chakuka katika shule ya Sekondari ya Kibasila.
Amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan,imetoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya sekta ya elimu ukiwemo ujenzi wa mabweni hayo ili kusaidia watoto wa kike,wakiwemo wa kiume kupata elimu bora na ya uhakika.
Amesema haiwezekani serikali iwezekeze fedha nyingi katika ujenzi wa miundombinu ya elimu kisha juhudi hizo zikahujumiwa na baadhi ya watu wachache kwa kujihusisha na vitendo vinavyoweza kukatisha elimu kwa mtoto wa kike.
Kwa sababu hiyo mh waziri mkuu,amesema ameridhishwa na viwango vya ujenzi wa bweni na bwalo kwenye shule ya Sekondari ya Kibasila ambalo ujenzi wake umegharimu shilingi bilioni 1.13
Hata hivyi amewataka wote watakaolitumia jengo hilo walinde miundombinu yake ili litumike kwa muda mrefu
Waziri Mkuu amesema kuwa Rais Dkt. Samia amedhamiria kuendelea kutenga fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya elimu kote nchini.
Naye, Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke amesema kuwa kukamilika kwa jengo hilo kutasaidia wanafunzi wa kike 228 hasa wa kidato cha tano na sita kupata elimu bora katika mazingira ya karibu hivyo kusaidia kuongeza ufaulu.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam John Chalamila,amemshukuru mh Rais kwa kutoa fedha nyingi za utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika mkoa wake ikiwemo wilaya ya Temeke.




Comments
Post a Comment