Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini Mhadisi Victor Seff amesema wakala huo mikoa mbalimbali inaendelea na kazi za matengenezo kwenye barabara zinazounganisha miji na vijiji nchini.
Matengenezo ya miundombinu yapo kwenye hatua mbalimbali kwa mwaka huu wa fedha ambapo moja ya maeneo yenye ukarabati na matengenezo alilotembelea hivi karibuni ni Wilaya ya Mkalama Mkoa wa Singida.
Mhandisi Self amesema Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Wilaya ya Mkalama mkoani Singida inaendelea na ujenzi pamoja na matengenezo ya barabara na madaraja ili kuhakikisha wananchi wanazifikia huduma za kijamii na kiuchumi kwa urahisi.
Naye Meneja wa TARURA katika Wilaya hiyo, Mhandisi Rahabu Thomas amesema kuwa hadi sasa miradi mbalimbali imekamilika ikiwemo ujenzi wa barabara ya Gengerankuru - Moma yenye urefu wa mita 640 kwa kiwango cha lami pamoja na kuweka taa.
Mhandisi Rahabu amesema kuwa barabara hiyo imewasaidia wananchi hasa kipindi wanapohitaji kupata huduma katika Ofisi za Serikali kwani wanafika kwa urahisi.
Aidha ameeleza kuwa mradi mwingine uliokamilika ni ujenzi wa Barabara na madaraja katika Barabara ya Iguguno - Lyelembo - Msingi yenye urefu wa Km 4.33 ambapo pia amesema kuwa barabara hiyo inarahisisha shughuli za kiuchumi kwa wananchi.
"Barabara hii ni muhimu kwa wananchi kwani sasa wanasafirisha mazao na kuzifikia huduma za kijamii kiurahisi", amesema Mhandisi Rahabu.
Naye Grace Benjamini mkazi wa kijiji cha Ilansoni amesema kuwa hapo awali mazao yao yalikosa soko la uhakika lakini kutokana na kukamilika kwa barabara hiyo sasa mazao yao yamepata soko na bei imepanda.
"Kutokana na barabara hii kupitika sasa mazao yanafika sokoni kwa urahisi na bei imeongezeka na wananchi wanapata faida", amesema Grace



Comments
Post a Comment