Na Shomari Binda-Musoma
MKUU wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi amepongeza kazi nzuri inayofanywa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Mara Ghati Chomete kuwatumikia wanawake na wananchi.
Pongezi hizo amezitoa leo septemba 24 baada ya kutembelewa ofisini kwake na mbunge huyo na kufanya nae mazungumzo.
Amesema anatambua mchango mkubwa unaofanywa na mbunge Ghati Chomete akiwa bungeni na kwenye ziara zake mkoani.
Mtambi amesema katika vikao vya bunge amekuwa akichangia masuala mbalimbali yenye malengo ya kusaidia wananchi na kupatiwa ufumbuzi.
Amesema licha ya michango yake bungeni lakini amekuwa akifanya ziara kwenye mkoa mzima wa Mara kwa kuzungumza na kuchangia masuala ya kijamii.
" Nikupongeze na kukushukuru sana mheshimiwa mbunge kwa kazi nzuri unayoifanya katika kuwasemea wananchi ukiwa bungeni.
" Mchango wako tunauona na kuuthamini ukiwa bungeni na hata kwenye ziara zako unazokuwa ukizifanya kukutana na wananchi hongera sana kwa kazi nzuri",amesema.
Kwa upande wake mbunge wa viti maalum mkoa wa Mara Ghati Chomete ili kumsaidia Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoifanya ni kuweza kutenda kwa kushirikiana.
Mbunge Ghati amemshukuru mkuu wa mkoa wa Mara Evans Mtambi kwa kuufanya mkoa wa Mara kuwa wamoja na kushirikishana kwenye kila jambo la kimaendeleo.

Comments
Post a Comment