Ujenzi wa chuo kikuu cha Dodoma(Udom) kampasi ya njombe kuinua uchumi wa njombe

GEORGE MARATO TV
0




Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini Deo Mwanyika amesema kuwa ujenzi wa Chuo kikuu cha Dodoma(UDOM)Kampasi ya Njombe utaleta manufaa mengi ikiwemo kusogeza huduma ya elimu karibu na wananchi pamoja na kuinua uchumi wa Njombe. 

Mwanyika ameyasema hayo Septemba 20, 2024 wakati Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda akikagua utekelezaji wa miradi mbalimbali katika jimbo la Njombe Mjini.

Mwanyika amewataka wananjombe kujiandaa kwa ongezeko la fursa mbalimbali ambazo zitainua uchumi wakati na baada ya  kukamilika kwa ujenzi wa Chuo Kikuu  Njombe. 

Pia amewaasa wananjombe kuanza kuboresha nyumba za makazi na mahitaji mengine ambayo ni hitaji kwa uwepo wa Chuo Kikuu Njombe ifikapo 2027.

Aidha, Mhe. Mwanyika ameishukuru serikali kwa ujenzi wa barabara ya Mabatini - Ramadhani yenye urefu wa kilometa 1.46 kwa kiwango cha lami ambayo imegharimu zaidi ya shilingi milioni 600 na kiasi cha milioni 70 zimetengwa kwa ajili ya kufunga Taa katika barabara hiyo.

Pamoja na mambo mengine,Mwanyika ametumia ziara ya Waziri Prof.Mkenda kumshukuru Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali katika sekta ya Elimu, Afya, Maji, Nishati, Barabara, kilimo na Mifugo ikiwa ipo miradi iliyokamilika na kuanza kutoa huduma kwa jamii na ipo inayoendelea na ujenzi kwa hatua mbalimbali.

"Hakika Mhe. Rais kwa sehemu kubwa  amejibu vilio vya wananjombe kwa kuendelea kutekeleza miradi mbalimbali kisekta kwani miradi mingi imekamilika na miradi mingine anaendelea kuleta fedha kwa ajili ya ukamilishaji wa miradi hiyo kama ya Maji, barabara na usambazaji wa umeme katika vitongoji"alisema Mwanyika 

Hali kadhalika amewarai wananchi wa jimbo la njombe Mjini kuwa na moyo wa subira wakati serikali ikiendelea kuleta fedha za ukamilishaji wa miradi hiyo sanjari na kuwahimiza wananchi wa jimbo hilo kujiandaa kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba 2024. 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top