DARAJA LA MAGUFULI MBIONI KUKAMILIKA

GEORGE MARATO TV
0

 

Ujenzi wa Daraja la JP MAGUFULI unaotekelezwa na serikali katika ziwa Victoria eneo la kigongo-Busisi Mkoani Mwanza kwa gharama ya zaidi ya shilingi billioni mia saba umefikia asilimia 90.5

Daraja hilo la kwanza kwa urefu katika nchi za afrika mashariki na kati litakuwa kiungo muhimu cha usafiri na usafirishaji baina ya mikoa ya kanda ya ziwa pamoja na mataifa Jirani ikiwemo UGANDA,BURUNDI,RWANDA na JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO.

Meneja wa wakala wa Barabara nchini(Tanroads)Mkoa wa Mwanza Mhandisi AMBROSE PASCHAL amesema kuwa Daraja la JP MAGUFULI linajengwa kwa kutumia Teknolojia kisasa ya ujenzi wa madaraja marefu Juu ya Maji.

Mhandisi PASCHAL amesema kuwa Daraja hilo litakuwa na uwezo wa kubeba Tani 120 za Mizigo na linatarajiwa kuanza kutoa huduma ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

Daraja la JP MAGUFULI linajengwa na Mkandarasi wa kampuni ya CHINA CIVIL ENGINEERING CONSTRUCTION CORPORATION(CCECC)ya nchini china ambayo imeeleza kuvutiwa na mazingira mazuri ya kisiasa pamoja na sera bora za uwezaji nchini.

Meneja wa Mradi huo kutoka kampuni ya CCECC,Mhandisi LI GUOJUN ameeleza kuwa mazingira mazuri ya kisiasa pamoja na sera bora za uwekezaji yamewawezesha kutekeleza majukumu yao ya ujenzi wa daraja hilo kwa ufanisi zaidi.

Mhandisi Guojun amesema kuwa kampuni hiyo inajivunia kurithisha teknolojia iliyotumika kwenye ujenzi wa daraja la JP Magufuli kwa vijana wa kitanzania wakiwemo wakandarasi wazawa na matumaini yake ni kwamba wataitumia teknolojia hiyo kwa manufaa ya Taifa.

Kwa upande wao,vijana wakitanzania  walionufaika na Teknolojia hiyo wameishukuru serikali na kampuni ya CCECC kwa kuwapa fursa ya kufanya kazi kwenye mradi wa ujenzi wa daraja la JP Magufuli.

Vijana hao wamesema kuwa ujuzi wanaoupata utawawezesha kutoa mchango kwenye maendeleo ya Taifa ikiwemo kutekeleza kwa ukamilifu miradi ya ujenzi wa madaraja marefu.

Daraja la JP Magufuli lina urefu wa kilometa tatu pamoja na upana wa mita 28.4 na litakuwa kiungo muhimu cha usafiri na usafirishaji pamoja na kuchochea ukuaji wa uchumi kupitia sekta ya uchukuzi.

Kukamilika na kuanza kutoa huduma kwa Daraja hilo ifikapo desemba 31 mwaka huu kutaondoa adha kubwa kwa watumiaji wa kivuko cha Kigongo-Busisi

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top