Chuo cha maendeleo ya Jamii ufundi(CDTI) Misungwi mkoani Mwanza kinahitaji zaidi ya shilingi billioni 1.9 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa bweni la wasichana.
Kukamilika kwa ujenzi wa bweni hilo kutakifanya chuo hicho kuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 352 kwa wakati mmoja.
Makamu Mkuu wa chuo cha CDTI Misungwi Taaluma DONGO NZORI amebainisha hayo wakati wa ziara ya Naibu katibu mkuu wa wizara ya maendeleo ya Jamii,Jinsia,wanawake na makundi maalum FELISTA MDEMU,ambapo pamoja na mambo mengine amepata nafasi ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo.
Mradi wa ujenzi wa bweni hilo unatarajia kugharimu shilingi billioni 2.2 hadi kukamilika kwake ambapo litakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi wa kike 352.
Akizungumza wakati wa kukagua mradi wa ujenzi wa bweni hilo,Naibu Katibu Mkuu MDEMU amesisitiza dhamira ya serikali ya kukamilisha ujenzi huo.
Aidha ameiasa Jamii kuchangamkia fursa za masomo zinazopatikana kwenye chuo cha maendeleo ya Jamii ufundi Misungwi.
Katika kituo kikuu cha mabasi nyegezi Jijini mwanza, Naibu katibu mkuu wa wizara ya maendeleo ya Jamii,Jinsia,wanawake na makundi maalum FELISTA MDEMU amepongeza uanzishwaji wa kamati ya ulinzi wa mtoto.