Na Robinson Wangaso - Mwanza.
Mashirika yanayo jishughulisha na utetezi wa Haki za Binadamu nchini Tanzania yaliyo chini ya mtandao wa THRDC wamehimizana kuendendelea na utetezi kwa kukemea na kutoa taarifa za vitendo vya matukio ya upoteaji wa watoto unaoendelea hapa nchini.
Kauli hiyo imetolewa jijini Mwanza na washiriki wa mafunzo na siku nne na mkutano mkuu wa Kanda ya ziwa, unaoendelea katika hotel ya Gold Crest jijini Mwanza ambao ulianza Julai 23, 2024.
Mafunzo hayo yanahudhuriwa na washiriki wapatao 60 kutoka Mashirika yanayojishughulisha na utetezi wa haki za binadamu kutoka mikoa ya Geita, Mwanza, Kagera, Shinyanga, Simiyu na Mara.
Awali akifungua mkutano huo Mratibu wa mtandao wa watetezi wa haki za binadamu nchini THRDC ndugu Onesmo Olengurumwa, alisema mtandao huo utajikita kukemea na kufichua vitendo vya ukatili na ukiukwaji wa haki za binadamu hapa nchini.
Katika hata nyingine, mratibu Onesmo amempongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan, Kwa maagizo yake juu ya hali ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini.
" Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan, katoa agizo kwa viongozi Serikali ngazi zote kushughulikia matukio ya upoteaji na wizi wa watoto. Agizo la mheshimiwa Rais ni letu sote tusikae kimya". Alisema Onesmo Ngurumo.
Amesisitiza na kuwahasa washiriki hao kuendelea kukemea vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu, ili kurejesha hali ya amani na kuondoa hofu inayotokana na utekwaji wa watu na upoteaji wa watoto.


Comments
Post a Comment