John Bina Ashauri Elimu ya Sheria na Kanuni za Madini itolewe Kwa Wananchi Ili Kuondokana na Migogoro Kati ya Wawekezaji na Wananchi
Rais wa shirikisho la wachimbaji wa madini nchini (FEMATA) Bw John Bina,amesema migogoro mingi kati ya jamii na wawekezaji katika sekta ya madini, inatokana na baadhi ya viongozi wakiwemo wa kisiasa kushindwa kuelewa vyema kutafasili sheria na kanuni zinazoongoza sekta hiyo.
Bw Bina ametoa kauli hiyo Jijini Dar es Salam, wakati akikabidhiwa vitetendea kazi zikiwemo camera video, kutoka kwa mkurugenzi wa kampuni ya uuzaji wa vifaa vya uchimbaji na mitambo ya Anyang Company Ltd ya jijini Mwanza. Ili kuimarisha utendaji kazi katika idara ya habari ya shirikisho hilo.
Kwa sababu hiyo rais huyo wa FEMATA nchini, ameiomba wizara ya madini na wadau wengine wa sekta hiyo, kutoa elimu juu ya sheria za madini na kanuni zake, hasa kwa viongozi wa ngazi za wilaya,madiwani katika maeneo yenye migodi wakiwemo wadau katika maeneo yao katika kuondoa migogoro na mivutano ambayo imechangia uhasama kati ya wawekezaji na jamii.
Kutokana na uwepo wa Changamoto hiyo amewaomba waandishi wa habari kutumia karamu zao vizuri kuandika vyema mambo yanayohusu migogoro katika sekta ya madini, ili kuepusha uvunjifu wa amani ktk maeneo hayo na kuwa tishio kwa uwekezaj mkubwa uliopo hivi sasa, ambao unaotokana na juhudi kubwa za serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Naye mkurugenzi mtendaji kampuni ya Anyang Co LTD ya jijini Mza Bw Henry Aron, amesema kampuni yake inayojihusisha na uuzaji wa vifaa vya uchimbaji wa madini na mitambo, ametoa vifaa hivyo kwa FEMATA kama sehemu ya kutambua mchango wa shirikisho hilo katika kukuza sekta ya uchimbaji wa madini, na hivyo kuamua kutoa shukrani zake katika kuimarisha kitengo cha habari cha shirikisho hilo.
Kwa upande wake mkuu wa idara ya habari wa FEMATA Dr Benard Joseph, akizungumza baada ya kupokea vifaa hivyo ametoa ahadi kutumia vifaa kwaajioi ya kutoa elimu inayohitajika kwa wachimbaji wa madini hapa nchini.



Comments
Post a Comment