Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya 3T inayotekeleza miradi ya kaboni ya upandaji miti, Bw. Solomon Yamoah (kulia kwake) wakati wa ziara yake nchini Ghana.
Katika mazungumzo yao, Mhe. Dkt. Kijaji amemhakikishia Bw. Yamoah kuwa Tanzania iko tayari kufanya kazi na kampuni hiyo ili kuhakikisha miradi ya kaboni inashika kasi na kuleta mafanikio katika hifadhi ya mazingira.
Waziri Dkt. Kijaji akiwa ameambatana na Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Christina Mndeme na ujumbe wa Tanzania yupo katika ziara ya mafunzo na kubadilishana uzoefu katika biashara ya kaboni nchini Ghana.

Comments
Post a Comment