Mbunge wa Tabora Mjini Ampongeza Mganga Mfadhili Hospitali ya Rufaa Kitete kwa Uboreshaji wa Huduma za Afya

GEORGE MARATO TV
0


MBUNGE wa Jimbo la Tabora Mjini, Mhe. Hawa Mwaifunga, amempongeza Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora (Kitete), Dkt. Joackim Eyembe, kwa jitihada kubwa anazozifanya katika kuboresha huduma za afya kupitia matumizi ya mapato ya ndani ya hospitali hiyo.

Akichangia bajeti ya Wizara ya Afya leo Mei 12, 2026 Bungeni jijini Dodoma, Mhe. Mwaifunga amesema uongozi wa hospitali hiyo umefanikiwa kuboresha miundombinu mbalimbali, ikiwemo ukarabati wa baadhi ya wodi pamoja na ununuzi wa vifaa tiba vya kisasa, hatua inayochangia kuongeza ubora wa huduma kwa wananchi.

Aidha, amesema hospitali hiyo imeanzisha kituo cha mazoezi (GYM) ndani ya hospitali, hatua inayolenga kuwahamasisha wananchi kufanya mazoezi ya mwili ili kupunguza magonjwa yasiyoambukiza kama shinikizo la damu, kisukari na magonjwa ya moyo.

“Jitihada hizi zinaonyesha dhamira ya kweli ya kuboresha afya za wananchi na kuimarisha mapambano dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza,” amesema Mhe. Mwaifunga.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top