Tanzania Kuendelea Kujitangaza Kimataifa Kwa Kunadi Fursa za Kiuchumi-Makonda

GEORGE MARATO TV
0

 


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe. Paul Makonda amesema Tanzania itaendelea kuingia kwenye macho na masikio ya Dunia, kwa kuendelea kuonesha fursa zote zilizopo katika sekta ya Utalii , Madini na kilimo pamoja na uwepo wa vipaji mbalimbali.

Hayo amebainisha mapema hii leo, Aprili 20, 2026 katika hafla fupi ya utilianaji saini wa makubaliano ya kuandaa mashindano ya Miss World 2027 ambapo waziri Makonda amesema kuwa zaidi ya wageni elfu ishiriki kutoka nje ya nchi wanatarajiwa kushiriki jijini Dar es Salaam.






Aidha, Makonda amewataka waandaaji wa mashindano mbalimbali ya walimbwende kutimiza ahadi wanazoziahidi kwa washiriki jambo ambalo linaweza kupunguza migogoro katika jamii kuhusu madai ya zawadi au vitu vilivyoahidiwa kwa washindi katika mashindano husika.

Sambamba na hilo Waziri Makonda amesema kuwa Tanzania inaenda kuandika historia ya kuwa ni nchi ya kwanza kuandaa mashindano hayo katika ukanda wa Afrika mashariki na kati huki ikiwa nchi ya pili kuandaa barani Afrika tangu ilipoanza kushiriki mwaka 1967.

Katika hatua nyingine, Makonda amesema kuwa mashindano ya Miss World 2027 yanatarajiwa kufanyika kwa muda wa siku 28, muda ambapo utachagizwa na ratibq mbalimbali za matukio ya burudani na mitindo ili kufungua fursa katika jamii katika kuonesha bunifu mbalimbali na kuongeza kipato.

Akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sixtus Mapunda amesema kuwa pamoja na ujio wa Miss World, serikali ya Tanzania inaendelea kufungua milango ya fursa kwa ujio wa AFCON 2027,huku akithibitisha kujipanga katika kuandaa mashindano ya Miss World 2027.

Naye, Muandaaji na Mkurugenzi wa Mashindano ya Miss World, Miss Julia Morley amewataka waandishi wa habari kujitoa katika kuutangazia Umma na Dunia juu ya uwepo wa mashindano hayo kimataifa huku akiisifu Tanzania kwa uzuri wake na sababu ya kukimbiliwa na mataifa mbalimbali dunia.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top