Bulaya ni Vitendo sio Maneno

GEORGE MARATO TV
0


 Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini, Mhe. Ester Amos Bulaya, amekabidhi mashine ya kunakili nyaraka (photocopy machine) katika Shule ya Sekondari Nyamakokoto, ikiwa ni sehemu ya jitihada zake za kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia kwa wanafunzi na walimu.

Katika hafla hiyo, Mheshimiwa Mbunge aliambatana na Diwani wa Kata ya Nyamakokoto Mhe. Lucas Daniel Marco ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bunda, Viongozi hao walisisitiza umuhimu wa vifaa vya kisasa katika kuinua kiwango cha elimu na kurahisisha upatikanaji wa nyaraka muhimu shuleni.




Utoaji wa mashine hiyo unatarajiwa kusaidia kupunguza changamoto ya uchapishaji wa mitihani, nyaraka za kujifunzia pamoja na kazi mbalimbali za kiutawala shuleni hapo.

*Imetolewa na:*

*Ofisi ya Mbunge*

*Jimbo la Bunda Mjini*

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top