Massaburi atoa milioni 10 WRC,Asisitiza mshikamano na maendeleo ya kiroho Kivule

GEORGE MARATO TV
0






Na,George Marato-Dar es salaam

MBUNGE wa Jimbo la Kivule, Ojambi Massaburi, ameonesha moyo wa kujitoa kwa jamii baada ya kuchangia shilingi milioni 10 katika Kanisa la The World of Reconciliation Church (WRC) wakati wa maadhimisho ya miaka 19 ya kanisa hilo yaliyofanyika Aprili 6, 2026, katika Kata ya Kivule.

Maadhimisho hayo yaliyovutia maelfu ya waumini na wananchi, yalifanyika chini ya uongozi wa Prophet Suguye, ambapo mbali na ibada, pia yaligeuka kuwa jukwaa la kuimarisha mshikamano wa kijamii na kiroho.

Akizungumza katika tukio hilo Leo April 6,2026, Massaburi ameeleza kuwa mchango huo ni sehemu ya kuunga mkono kazi kubwa inayofanywa na taasisi za dini katika kujenga maadili mema, kusaidia wahitaji na kuimarisha amani katika jamii.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Deus Clemence Sangu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano), ambaye amesisitiza nafasi ya makanisa na taasisi za dini katika kukuza maadili, nidhamu na mshikamano wa kitaifa.

Katika kuonesha umoja wa uongozi, Mbunge huyo aliambatana na madiwani wote wa Jimbo la Kivule, hatua iliyodhihirisha ushirikiano wa viongozi katika kusukuma mbele maendeleo ya wananchi.

Maadhimisho ya miaka 19 ya WRC yameacha alama ya kipekee kwa waumini na jamii kwa ujumla, yakionesha jinsi taasisi za dini zinavyoendelea kuwa nguzo muhimu katika maendeleo ya kijamii na kiroho.




Mwisho

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top