WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Aprili 6, 2026 anakagua madhara yaliyotokana na kuungua kwa soko la wafanyabiashara wadogo la Simu 2000, lililopo Ubungo jijini Dar es Salaam.
Ajali hiyo ya moto katika Soko hilo ilitokea Aprili 4 2026 ambapo inakadiriwa vibanda takribani 500 vya wafanyabiashara wadogo viliteketea kwa moto.








