Mwera na Tungamaa waitika ziara Katibu UVCCM Pangani

GEORGE MARATO TV
0


Na: Mwandishi Wetu, Pangani

Katibu wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilayani Pangani, Nasri Mkalipa, amepata mapokezi makubwa katika ziara yake Kata za Mwera na Tungamaa Machi 26, 2026, ikiwa ni siku ya tatu ya ziara yake ya ujenzi wa Chama wilayani humo. Katika ziara hiyo, Mkalipa amewaleza vijana hao namna serikali inavyotekeleza miradi ya maendeleo inayogusa maisha na vijana na wananchi.

"Serikali ya CCM ni ya vitendo si maneno, ikiahidi inatekeleza. Rais wetu Dk. Samia Suluhu Hassan ametoa shilingi bilioni 200 kwa vijana ziwasaidie katika kuinua hali zao za kiuchumi. Vijana na wananchi wa  Pangani tusilale, tuwe sehemu ya wanufaika wa fedha hizo," amesema Mkalipa.

Sambamba na hilo, Mkalipa amesema uhai wa Chama unategemea sana vijana, hivyo ni vyema vijana wakafanya juhudi kuongeza idadi ya wanachama kwani nguvu ya Chama ni wanachama wake. Katika ziara hiyo, vijana wamemshukuru Mkalipa kuwatembelea na kusikiliza changamoto zao huku wakiahidi kujitoa kwa ajili ya uhai na maendeleo ya Chama chao.





Ziara ya Katibu huyo iliyopewa jina la "Operesheni Samia" ni sehemu ya majukumu yake ambapo atatumia siku tisa kuzifikia Kata zote 14 za wilaya ya Pangani kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama, kusikiliza kero za wananchi na kuhimiza maendeleo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top