Kifo cha Lukuvi Chaahirisha Harambee Kubwa na Ufunguzi wa Kanisa Serengeti

GEORGE MARATO TV
0


 Taasisi ya Nyansaho foundation imehairisha hafla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa shule mpya ya msingi na Zahanati katika kijiji cha Musati, ambayo ilitarajiwa kuongozwa na Jaji mkuu wa Tanzania mh George Masaju. 

Hafla hiyo ambayo pia ingehudhuriwa na Waziri wa ujenzi mh Abdallah Ulega pamoja na mwenyekiti wa taasisi ya Nyansaho foundation mh Rhimo Nyansaho ilipangwa kufanyika machi 28 mwaka huu 2026 katika kijiji cha Musati Wilayani Serengeti mkoani Mara, sambamba na ufunguzi wa kanisa la Waadventista Wasabato Wasaba Musati Central katika eneo hilo. 

Taarifa iliyotolewa na taasisi ya Nyansaho imesema kuahirishwa kwa Shughuli hizo kunatokana kifo cha aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Watu Wenye Ulemavu) na Mbunge wa Jimbo la Isimani, Marehemu William Vangimembe Lukuvi (Mb)

 Taasisi ya Nyansaho foundation imesema itatangaza tarehe rasmi kwa AJILI ya kufanya zoezi hilo huku ikitoa pole kwa ndugu, Familia, Serikali na Watanzania wote kufuatia kifo cha kiongozi huyo. 

Mhe. Lukuvi amefariki asubuhi ya jana tarehe 25 Machi, 2026 katika Hospitali ya Benjamini Mkapa alipokuwa akipatiwa matibabu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top