Mkalipa Azidi Kuimarisha Uhai wa Ccm Pangani

GEORGE MARATO TV
0


Na: Mwandishi Wetu, Pangani 

Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Pangani, Nasri Mkalipa, ameendelea na ziara ya Operesheni Samia ikiwa ni mwendelezo wa Jumuiya anayoingoza kuhakikisha uhai wa Chama unaendelea kuimarika zaidi katika Kata zote 14 za wilaya ya Pangani.

Machi 25, 2026, Mkalipa amefanya ziara katika Kata za Kipumbwi na Mikinguni ambapo amekutana na wanachama wa CCM na wananchi hasa vijana ambao amewahimiza kuendelea kukitumikia Chama kwani Chama kipo pamoja nao bega kwa bega kuhakikisha changamoto zao zinapatiwa ufumbuzi.






"Serikali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ipo kazini kuhakikisha changamoto za vijana zinapatiwa ufumbuzi, anatoa fedha nyingi kwa ajili ya vijana, ni wajibu wenu kama vijana kujiunga katika vikundi ili muweze kunufaika na fursa mbalimbali zinazotolewa na serikali," amesema Mkalipa.

Aidha, Mkalipa amewahimiza vijana kudumisha amani na mshikamano kwani ndiyo nyenzo ya mafanikio. Kwa upande wa vijana, wameishukuru serikali kwa kuleta miradi mingi ya maendeleo katika Jimbo la Pangani inayogusa sekta za elimu, afya, maji, umeme, miundombinu, uvuvi na kilimo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top