Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Benki ya TIB Yapokea Ugeni kutoka EADB, Wafanya Ziara Pipes Industries


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Benki ya Maendeleo (TIB) leo ilimkaribisha rasmi Meneja Mkazi (Country Manager – Kenya) mpya wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (EADB), Bi. Angela Muga na ujumbe wake kwa ziara maalumu yenye lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya Taasisi za Fedha za Maendeleo (DFIs) katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Katika ziara hiyo iliyoambatana na ujumbe kutoka benki ya EADB, imeonyesha dhamira ya pamoja ya kuharakisha ukuaji endelevu wa uchumi, kubadilishana uzoefu, ujenzi wa viwanda na ujumuishaji wa kikanda katika eneo la Afrika Mashariki.

Ujumbe wa Bi. Muga ukiongozwa na mwenyeji wake Bw. Stephen Wambura ambaye ni Meneja Mkazi EADB Tanzania, pia ulipata nafasi ya kufanya ziara katika kiwanda cha kuzalisha mabomba ya plastiki cha Pipes Industries kilichopo eneo la viwanda la Vingunguti jijini Dar es Salaam ambapo kiwanda hicho ni mnufaika muhimu wa ufadhili huo wa pamoja.

Kiwanda cha Pipes Industries kilipokea mkopo wa takribani Shilingi za kitanzania Bilioni 28.65, ambao umekuwa na mchango mkubwa katika kupanua uwezo wake wa uzalishaji na kuimarisha shughuli zake.

Mtaji huo umeiwezesha kampuni kuongeza uzalishaji wa bidhaa muhimu za plastiki, ikiwemo mabomba yenye umuhimu mkubwa kwa miundombinu ya usambazaji wa maji mijini na vijijini.Kiwanda hicho kimeleta matokeo muhimu ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuzalisha ajira kwa Watanzania, kuongeza mapato ya serikali kupitia kodi na kuboresha upatikanaji wa vifaa vya miundombinu ya maji vinavyosaidia mitandao ya usambazaji wa maji.

Uwekezaji huu unaendana na mkakati mpana wa Tanzania wa ujenzi wa viwanda kwa kukuza uzalishaji wa ndani na kupunguza utegemezi wa bidhaa kutoka nje.

Kwa kuunga mkono kiwanda kama cha Pipes Industries, TIB inaendelea kuwa na mchango muhimu katika kuimarisha sekta binafsi na kuongeza ustahimilivu wa uchumi.

Akizungumza wakati wa ukaribisho huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo TIB, Bw. Deogratius Kwiyukwa, alisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya taasisi za fedha za maendeleo za kikanda katika kuhamasisha mitaji ya muda mrefu kwa ajili ya miradi yenye kuleta mabadiliko.

Kwiyukwa alisema, “Ni furaha kubwa kwetu kumkaribisha rasmi ofisini kwetu Bi. Angela Muga, Meneja Mkazi mpya wa Benki ya Maendeleo Afrika Mashariki (EADB Kenya).

Ushirikiano wetu huu ni wa muda mrefu zaidi ya miaka 10 ambapo kupitia EADB, TIB imeweza kutoa fedha za miradi zenye jumla ya thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 80 ambazo zimegawanywa kwenye sekta mbalimbali zikiwemo; kilimo, afya, elimu, viwanda, madini na utalii.”Kwiyukwa alisisitiza

“Kupitia ushirikiano huu, zaidi ya shilingi Bilioni 28 zimewekezwa katika mradi wa upanuzi wa Kiwanda cha Mabomba ya plastiki cha Pipes kilichopo Vingunguti Dar es Salaam ambapo matokeo ya uwekezaji hu oni pamoja na kuongezeka kwa uzalishaji wa bidhaa za plastiki kama mabomba ya maji, ajira kwa vijana wakike na wakiume na kukuza sekta ya viwanda nchini.”

Kwa upande wake, Meneja Mkazi wa Benki ya EADB Bi. Angela Muga alisema, “Ushirikiano miongoni mwa Taasisi za Fedha za Maendeleo ni muhimu katika kufungua fursa za mitaji mikubwa kwa ajili ya mabadiliko ya kikanda. Kwa kuoanisha rasilimali zetu tunaweza kuharakisha ukuaji wa viwanda, kuimarisha ujumuishaji wa kikanda na kuleta matokeo endelevu kwa Afrika Mashariki.”

Aidha aliongeza, “Mwenendo huu unaokua wa ushirikiano kati ya taasisi za fedha za maendeleo unaonekana kupitia juhudi za pamoja kati ya taasisi kama Benki ya Maendeleo ya TIB na EADB, ambazo zinaendelea kuhamasisha mitaji ya muda mrefu kwa ajili ya miradi yenye kuleta mabadiliko nchini Tanzania na katika ukanda mpana zaidi.”Ushirikiano kati ya TIB na EADB unaonesha kukua kwa nafasi ya taasisi za kifedha za kikanda.


Kwa kutoa mitaji ya muda mrefu yenye uvumilivu, taasisi hizi zinajenga minyororo muhimu ya kuongeza thamani ambayo inaendelea kuleta matokeo chanya hata baada ya kipindi cha ufadhili kumalizika.

Kuhusu Benki ya Maendeleo TIB, Benki ya Maendeleo TIB ni taasisi ya Serikali na ni ya kisera, imeundwa mahususi kwa ajili ya kuchochea maendeleo ya uwekezaji wa ndani ya nchi hususani katika kufanikisha utekelezaji wa miradi ya Serikali na miradi ya sekta binafsi.

Benki inalenga sekta za kipaumbele ikiwemo miundombinu, kilimo, viwanda na uzalishaji, madini, utalii, uchumi wa buluu pamoja na biashara ndogo na za kati (SMEs).

Aidha, Benki ina jukumu muhimu katika kusimamia mifuko ya maendeleo na kusaidia maandalizi ya miradi ili kuibua uwekezaji unaochochea ukuaji endelevu wa uchumi wa Tanzania.

Kuhusu EADB, Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (EADB) ilianzishwa mwaka 1967 chini ya mkataba wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati huo. Dhamira yake ilikuwa kutoa msaada wa kifedha na huduma zinazohusiana kwa makampuni katika nchi wanachama ambayo, kupitia shughuli zao, yalitarajiwa kutoa mchango chanya katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika ukanda huo. Benki ilianzishwa upya chini ya Hati mpya mwaka 1980.

Chini ya Hati hiyo, jukumu na dhamira ya Benki vilipitiwa upya na wigo wa shughuli zake kupanuliwa kujumuisha huduma mbalimbali za kifedha katika nchi wanachama, ikiwa na lengo kuu la kuimarisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi pamoja na ujumuishaji wa kikanda. Kwa sasa, EADB inamilikiwa na nchi nne wanachama ambazo ni Kenya, Uganda, Tanzania na Rwanda pamoja na taasisi nyingine za maendeleo na kifedha za kibiashara. 

Ikiwa ni chombo cha Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na kupitia ushirikiano wake na taasisi za EAC, imepata jukwaa la kuchochea ujumuishaji wa kikanda kupitia utoaji wa fedha za maendeleo.

Comments

#maratotv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

Wananchi Serengeti Wamtaja Dkt Rhimo Nyansaho Kama Chachu ya Maendeleo Kwao

Na Shomari Binda-GMTV  WANANCHI Wilaya ya Serengeti mkoani Mara wamemtaja Dkt.Rhimo Nyansaho kama chachu ya maendeleo kupitia taasisi yake ya Nyansaho Foundation. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na GMTV wananchi hao wamesema kwa kipindi kirefu mchango wake umeonekana katika kuisaidia jamii. Wamesema ukifika Jimbo la Serengeti kila Kata na Kijiji huwezi kukosa mkono wa Dkt.Nyansaho kuchangia na kusaidia jamii kuanzia elimu,afya,maji na masuala mengine ya jamii. Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Mwita Sagati amesema wapo watu wanaojitokeza kusaidia jamii kipindi cha uchaguzi kwa kulenga kupata uongozi lakini imekuwa tofauti kwa Dkt.Nyansaho. Sagati amesema iwapo atajitokeza kuomba nafasi ya ubunge wapo tayari kumpambania na kumchagua ili aweze kuendelea kutoa mchango wake katika kusaidia jamii. " Tunashukuru sana mchango wa Dkt.Nyansaho kwa kuchangia shughuli za maendeleo hapa Serengeti. " Wengine huwa wanakuja nyakati za uchaguzi lakini huyu mchango wake ni ...

MAKOMANDOO MIAKA 60 YA JWTZ,HAIJAWAHI KUTOKEA

Makomandoo ya jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)wamekuwa kivutio cha aina yake kwenye kikele cha maadhimisho ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo. Katika sherehe hizo ambazo zimefanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja huo wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 1 Septemba, 2024. Rais ameonesha kujivunia na kulipongeza JWTZ kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza Marais waliomtangulia kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wa uongozi wao kwa kuliongoza vema jeshi hilo.

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...

Jenerali Jacob Mkunda Atembelea Meli Tiba ya China Aridhishwa na Huduma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea meli tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika. Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ . Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ  na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China. Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini tarehe 23 Julai mwaka huu.

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...