WAZIRI Mkuu mstaafu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amemuelezea Hayati Rais John Magufuli kuwa ni mtu mkali, ambaye hakupenda mzaha katika mambo yake, alikuwa mchpakazi, Mzalendo na alikuwa kiongozi Mwenye akili nyingi katika kutekeleza Majukumu yake kiufasaha.
Amesema Uzalendo unajengwa Kwa unajengwa na uwajibikaji.
Waziri Mkuu Mstaafu kasimu Majaliwa ameyasema hayo leo katika kumbukizi ya miaka mitano ya kifo cha Hayati rais Dk.John Magufuli Machi 17 katika viwanja vya makazi yake Chato mkoani Geita, Majaliwa amewataka Watanzania kuiga mambo mazuri yaliyofanywa na kiongozi huyo.
Amesema yeye alikuwa ni mtu mkweli, hakuwa na mzaha katika mambo yake yaani mkali , alikemea maovu, wezi, wala rushwa, wabadhirifu wa mali za umma, na yule ambaye hakufuata misingi hii aliachana nae huo ndiyo ulikuwa utaratibu wake
“Leo hii tunamkumbuka Hayati Magufuli, sisi ambao tulikuwa karibu naye tumeweza kushuhudia wakinufaika na busara zake, hekima zake katika kuongoza taifa hili, na kutambua rasilimali za nchi na wananchi wenyewe na wanyonge wakiwemo,” amesema Majaliwa.
Majaliwa amesema Magufuli alikuwa ni mchapakazi, mtu mwenye akili za ndani ya darasa, lakini pia hata nje ya majukumu yake, na alikuwa kiongozi mzalendo aliyejengwa na uwajibikaji, uaminifu, uadilifu na mpenda maendeleo.
Aidha, Majaliwa amesema wamenifunza mengi kutoka kwa hayati Magufuli ambapo hivi Sasa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani anatekeleza Miradi yote aliyoiacha Hayati Magufuli.
"leo Tukiwa hapa tunatambua watanzania kwamba tumempoteza kiongozi Mashuhuri, yupo Kwenye mioyo yetu, tuendelee KUMUENZI Kwa mazuri aliyotenda katika Taifa hili. na Tumuombee wote ili Mwenyezi Mungu aendelee kumuweka mahali pema Peponi". Amesema.
kumbukizi ya Miaka Mitano ya kumkumbuka Hayati John Pombe Magufuli imehudhuriwa na viongozi Mbalimbali huku Dr. Emmanuel Nchimbi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akimwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Wakati huo huo wa Makamu wa Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amesema kuwa, hayati magufuli alimfundisha kumtegemea Mungu kwenye majukumu yake ya kila siku.
Akizungumza leo wakati wa ibaada ya Kumbukizi ya Miaka mitano ya Kifo cha Hayati Pombe Maguguli iliyofanyika Wilayani Chato, Mkoani Geita, Dkt.Mpango amesema alibahatika kuwa mmoja wa wasaidizi wake, na alisisitiza zaidi kufanya kazi kwa weledi na kumtegemea Mungu katika kila jambo.
Aidha, amesema wakati alipougua, hayati Magufuli alimtaftia Masista kutoka Karagwe kwaajili ya Kumfanyika Maombi.
"Naomba watanzania wenzangu, tulishike hili kwani ni fundisho kubwa na tujifunze, Mtu asijifanye yeye ni Mtu mjanja sana,kumtegemea Mungu ni Maarifa Makubwa sana". Amesema
Aidha,.Amesema Hayati Maguguli alimwagiza asimamie Matumizi ya Serikali na hakuwa na mchezo katika uongozi wake.
Sambamba na Hayo amemwambia Mama Janeth Magufuli pamoja na familia Kwa ujumla kuwa Taifa lipo pamoja na yeye.
Ikumbukwe kuwa Hayati Magufuli alifariki Machi 17, 2021 katika hospitali ya Mzena, Dar es salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.



















