FCC Kusimamia Sheria Katika Kuwalinda Watumiaji wa Bidhaa Nchini

GEORGE MARATO TV
0


 DODOMA 

SERIKALI kupitia Tume ya Ushindani FCC imewahakikishia watanzania kwamba itaendelea kusimamia kikamilifu Sheria ya Alama za Bidhaa ili kuwalinda watumiaji dhidi ya bidhaa zisizo salama au zisizo halisi, na hivyo kupunguza hasara za kiuchumi zinazotokana na udanganyifu. 

Aidha, Kudhibiti bidhaa bandia kwa mujibu wa sheria kunachangia ukuaji wa uchumi. 

Kauli hiyo imetoleo leo jijini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC), Bi. Khadija Ngasongwa, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu miradi ya maendeleo na fursa kwa vijana.



Amesema kusudio hilo la serikali ni kuzifanya Biashara halali zinabaki na mapato yao, jambo ambalo litapelekea kuchochea uwekezaji zaidi, kuongeza ajira, na kuendeleza ubunifu. 

"Bidhaa bandia huzuia ushindani wa haki, kuathiri vibaya biashara halali, na kuhadaa watumiaji, hivyo kuunda uwanja usio sawa wa biashara". Amesema 

"Jitihada za kuzuia bidhaa bandia zinaboresha sifa ya biashara kitaifa na kimataifa, kuwavutia wawekezaji, na kuongeza mauzo ya nje". Ameongeza

Aidha, Bi.khadija amesema FCC imeendelea kutatua malalamiko ya walaji ambapo, katika robo ya kwanza na ya pili malalamiko 63 yalishughulikiwa na Kati ya malalamiko hayo, 45 yalipatiwa ufumbuzi na malalamiko 19 yaliyobaki yapo katika hatua mbalimbali za utatuzi.

‎Amesema kuwa pamoja na kushughulikia malalamiko, Tume hiyo pia ina jukumu la kusajili mikataba mbalimbali kwa mujibu wa sheria ambapo mikataba hiyo hupitiwa ili kuhakikisha inazingatia taratibu na kulinda maslahi ya walaji pamoja na sekta ya kifedha.

‎Kadhalika, amebainisha kuwa taasisi za fedha hasa katika sekta ya mikopo ya kifedha haziruhusiwi kuongeza riba au kufanya mabadiliko katika programu zao bila kupitia Tume ya Ushindani kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa.

Sanjari na hayo Tume ya Ushindani imekuwa ikifanya ushirikiano mkubwa na Benki Kuu ya Tanzania kwa kuwakutanisha wadau mbalimbali kujadili namna ya kuwalinda walaji hasa katika sekta za kifedha ambazo zimekuwa zikilalamikiwa na wananchi.


‎Amesema kuwa ushirikiano huo umefanyika kwa lengo la kuboresha huduma jumuishi za kifedha kupitia mifumo madhubuti ya kushughulikia malalamiko ya wateja ili kuhakikisha wanapata huduma bora.


‎Vile vile amebainisha kuwa katika kuboresha huduma kwa wananchi, Tume imefanya ushirikiano na Wakala wa Vipimo pamoja na wadau wengine kufuatilia malalamiko ya watumiaji wa huduma za intaneti ambapo wananchi wengi wamekuwa wakilalamikia matumizi ya vifurushi vya data.

‎Amesema kuwa tafiti zinafanyika ili kuhakikisha wananchi wanapata thamani halisi ya fedha wanazolipia kulingana na huduma wanazotarajia.

Hatua zote zilizofanywa na FCC ni kutokana na Maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani katika kusaidia kukuza uchumi wa nchi kwa kuhakikisha ushindani huru na wezeshi unaimarika pamoja na kuimarisha uchumi wa soko.




Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top