Hayo amebainisha leo, machi 3, 2026, jijini Dar es Salaam na Wakili Gido Thomas Simfukwe wakati akitoa mrejesho wa usikilizwaji wa mashauri ya mgawanyo wa mali na shughuli za kisiasa katika kesi NA. 8323 ya mwaka 2025 iliyofunguliwa na Saidi Issa Mohammed na wenzake dhidi ya chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) ambapo amesisitiza kuwa kupanga, kutangaza na kuandaa makongamano na mikutano ya kisiasa si sahihi kwani yamezuiliwa kwa amri ya Mahakama tangu tarehe 10 juni 2025.
Aidha, wakili Simfukwe amesema kuwa kumekuwa na baadhi ya watu wamekuwa wakitia dhana ya kuwa shauri hilo lililetwa na kikundi cha watu wachache hali ambayo si sahihi bali ni uwepo wa wanachama wenye nia ya kuona chama kinakuwa katika mikono ya wanachama.
Katika hatua nyingine Wakili Simfukwe amesema kuwa kitendo cha wanachama wa Chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) kusema kuwa zuio limekoma kutokana sababu kadhaa ni kupotosha jamii juu ya maamuzi ya mahakama yaliyotolewa.
Kwa upande wake Saidi Issa Mohammed ambaye ni mfungua shauri amesema kuwa hii kesi ni dai la wanachama na viongozi waandamizi wa chama kutoka zanzibar .
Sambamba na hilo Saidi Issa Mohammed amewaasa wanachadema kuvuta subira katika kipindi hiki huku akisema tabia inayofanya na viongozi wa chama kutaka kupinga amri ya mahakama ni kutaka kufunika madai ya viongozi na wanachama wa zanzibar juu ya haki ya msingi iliyowasilishwa mahakamani.
Hata hivyo ameeleza kuwa upotoshwaji unaoendelea hivi sasa katika chama unaweza kukifikisha chama katika hali mbaya sana kutokana na mwenendo wa shauri hilo tangu lifunguliwe mahakqmqni hapo.








