Mbunge Agness Aunga Juhudi za Rais Samia Kwa Kuwezesha Vijana Kwa Vitendo

GEORGE MARATO TV
0


 MUSOMA.

KATIKA kuunga mkono jitihada za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuwawezesha vijana,Mbunge wa viti maalumu mkoa wa mara Mhe, Agness Marwa amegawa vitendea kazi vya saloon za kike na kiume Kwa vijana zaidi 30 katika manispaa ya Musoma mkoa wa Mara.


Dhamira hiyo ni kuwawezesha vijana kujikwamua kiuchumi na kuunga mkono serikali katika kuwawezesha wajasiriamali wadogo.

Akizungumza katika kikao cha wajasiliamali leo March 3,2026 katika Manispaa ya Musoma, Mbunge Agnes amesema ataendelea kuyafukia makundi mablimabli wakiwemo wajasiliamali Mali wote katika mkoa wa mara.


Mhe. Agnes amesema azma hiyo ni kuunga mkono jitihada za mheshimiwa rais Samia Suluhu Hassan zinazojikita kuwasaidia wajasiliamali wadogo wadogo katika kujikwamua kiuchumi.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Manispaa ya Musoma Juma Chikoka amempongeza Mbunge huyo ambapo amewataka wajasiliamali hao kuvitumia vifaa hivyo Kwa Lengo lililokusudiwa ili kujiongezea kipato.


Nao baadhi ya wajasiliamalia mali wamempongeza na kumshukuru Mbunge Agnes Kwa Kutoa vifaa hivyo kwani vitakwenda kutatua changamoto zilizokuwa zikiwakabilia za upungufu wa vifaa kulingana na kipato kidogo wanachopata ambacho hakikidhi mahitaji ya kununua vifaa hivyo Kwa wingi.



vifaa vilivyotolewa na Mbunge Agnes ni pamoja na Mashine za kunyolea, draya na mtaji wa kununulia vifaa kazi vya saloon kama vile shampoo. 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top