Kijana huyu alizaliwa Julai 4, 1983 huko Mtwara. Akasoma shule ya msingi Shangani iliyopo Mtwara Mjini kuanzia 1992 hadi 1998. Mtihani wa darasa la Saba akashika nafasi ya tatu kiMkoa. Akachaguliwa kujiunga kidato cha kwanza shule ya sekondari ya vipaji maalumu Kibaha, Pwani. Mwaka 2000 akafanikiwa kuingia kumi bora mtihani wa kidato cha pili kwa kanda ya mashariki, akaongoza masomo mawili ikiwemo Hisabati.
Mwaka 2002 akahitimu kidato cha Nne kwa kupata alama “A” katika masomo tisa kati ya kumi aliyofanya katika mtihani wa taifa. Baraza la Mitihani “NECTA” likamtangaza Joel kuwa Mwanafunzi bora kitaifa. Akachaguliwa kuendelea sekondari Kibaha, Mchepuo wa PCB. Akahitimu kidato cha sita na kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es salaam kusomea shahada ya Biashara na Uongozi. Baadae akasoma stashahada ya juu ya Diplomasia ya Uchumi (post-graduate in economic diplomacy). Badae akasoma shahada ya uzamili ya maendeleo na uhusiano wa kimataifa (International cooperation and development).
Anajulikana kwa kazi zake za kutoa mafunzo ya biashara na uongozi. Ameandika vitabu 45 na amewahi kutajwa kuwa miongoni mwa vijana 100 wenye ushawishi zaidi barani Afrika. Amewahi kutunukiwa tuzo na taasisi ya ICN ya nchini Marekani kwa kutambua mchango wake wa kuleta mabadiliko kwa watu nchini Tanzania.
Mwaka 2024 alitunukiwa shahada ya heshima ya uzamivu katika Uongozi na Usimamizi wa Biashara (PhD in Leadership and Business Management) na Chuo Kikuu cha Veridian kilichopo Atlanta, Georgia, Nchini Marekani.
Mwanzilishi wa shirika lisilo la kiserikali la Joel Nanauka Foundation lenye maono, lililojitolea kuboresha maisha ya watu wasio na fursa. Akagusa maisha ya wanyonge wengi. Mwaka 2010, akiwa na umri wa miaka 27, akagombea Ubunge Jimbo la Mtwara Mjini kupitia CCM lakini hakufanikiwa. Mwaka 2015 akagombea tena Ubunge kupitia CHADEMA pia hakufanikiwa. Hatimaye mwaka 2025 akachaguliwa kuwa Mbunge wa Mtwara Mjini kupitia CCM na ikampendeza Mhe.Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kumteua kuwa Waziri wa Vijana.
Hili ni moja ya zao bora la Uongozi lililopandwa katika Nchi yetu. Mtumishi wa Mungu, Mwalimu, kiongozi, mshauri na rafiki wa wengi. Kijana smart, Makini na mwenye fikra tunduizi.👏
Waziri wa Vijana Dkt Joel Nanauka




