📌 *Wananchi wahimizwa kujiunga mapema na huduma ya umeme* .
📌 *Wananchi waaswa kutumia huduma ya umeme kwa tija* .
📍 *MKINGA*
Wakala wa Nishati Vijijini (REA) unaendelea kufanyia vitendo nia yake ya kujali na kuthamini wananchi kwa kusaidia inafikisha huduma nafuu ya umeme kwenye kila kijiji na kijiji mkoani Tanga ili huduma hiyo isaidie kuboresha maisha ya wananchi mkoani humo.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa maendeleo ya jamii kutoka REA, ndugu Abdulrazack Mko wakati wa ziara ya kuhamasisha wananchi kujiunga na huduma ya umeme wilayani Mkinga mkoani Tanga.
Aidha Mkomi, amewasisitiza wananchi kuwa waangalifu wakati wa kufanya malipo ya kujiunga na huduma ya umeme, akieleza kuwa gharama ya kuunganisha umeme vijijini ni shilingi 27,000 kwa makazi na shilingi 139,000 kwa Mitambo na mashine au viwanda na malipo yote yanalipwa kwa kutumia kumbukumbu inayotumwa moja kwa moja kutoka TANESCO kwa njia ya meseji na si vinginevyo.
Aidha, uhamasishaji huo ulijikita zaidi katika kutoa elimu kwa wananchi ya namna ya kujiunga na huduma ya umeme na matumizi ya umeme yenye tija kutumika kufanya biashara kama saluni, uchomeaji, viwanda na nyingine nyingi ambazo zitasaidia kuongeza ajira na kipato.
Hali ya wananchi wameaswa kushiriki katika utunzaji wa miundominu inayojumuisha nguzo, nyaya na uhusiano mwingine wa umeme ili kuomba unaoweza kurejesha huduma ya umeme pamoja na kuhatarisha usalama wa watu pamoja na mali.
*Mwisho* .



