_Aagiza ijengwe na TANROADS ili iwe bypass ya kupunguza msongamano mjini._
Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba leo Februari 20, 2026 amekagua ujenzi wa barabara ya Spencon-Mabogini-Kahe-Chekereni yenye urefu wa kilomita 31.25.
Akizungumza na Wananchi wa Mabogini, Wilaya Moshi Mkoani Kilimanjaro, Dkt. Mwigulu ameelekeza barabara hiyo ihamishwe kutoka TARURA, na kwenda TANROADS ili ijengwe kwa kiwango cha lami kwa kuwa ni Bypass hivyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza msongamano katikati ya mji wa Moshi.






