Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba leo Februari 12, 2026 amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika maadhimisho ya miaka 30 ya Taasisi ya Saratani Ocean Road.
Maadhimisho yanayofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam yanatoa fursa kwa Taasisi hiyo pamoja na wadau wengine kutafakari kwa pamoja safari ya mapambano dhidi ya saratani kwa kuangalia walipotoka, walipo na wapi wanaelekea.






