Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Lameck Nchemba leo Januari 31, 2026 ameshiriki kwenye Azania Bank Bunge Bonanza 2026 linalofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya John Merlin jijini Dodoma ambapo ametumia nafasi hiyo kuwashukuru Azania Bank kwa kuendelea kuzamini Bonanza hilo.
Amesema Bonanza hilo limefana sana kutokana Azania Bank kulipamba na mwitikio wake ni mkubwa.
Akizungumza Mara baada ya kumaliza Matembezi, Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu ametoa rai kwa watanzania kuweka ratiba ya kufanya Mazoezi kwajili ya Afya zao pamoja na kuleta umoja wa Kitaifa.
"Nitoe Rai Kwa watanzania kuweka ratiba ya kufanya Mazoezi kwajili ya Afya zao na kuleta umoja Kwa Kitaifa, na kufanya Mazoezi ni jambo jema la Afya, hivyo Kila mmoja atenge Muda wake Afanye mazoezi ili kuondokana na Magonjwa yasiyo ya kuambukiza". Amesisitiza
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania Dkt. Esther Mang'enya amesema pamoja na Kuwezesha uchumi lakini pia Azania Bank inawezesha Afya za watu kwa kuendelea Kutoa huduma mablimabli hususani kwenye sekta ya Michezo ili kuwafanya watanzania kuipenda Michezo kama sehemu yao ya kuimarisha Afya zao.
"Ni mwaka wa tatu mfululizo Sasa ofisi ya Bunge kutupa nafasi ya kuwa wadhamini wa Bunge Bonanza na LA mwaka huu linaitwa Azania Bank Bunge Bonanza 2026". Amesema
"Sisi kwetu ni fahari kupata nafasi hii ya kushiriki kama wadhamini Kwa sababu Michezo ni kitu kikubwa sana ambacho kinaunganisha watu,Kusalimiana pamoja na kuwa kitu kimoja". Ameongeza.
Kadhalika, amesema wao kama Bank pia wanajikita kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja pamoja na uchumi wa nchi ambapo amezitaka na taasisi zingine Kushirikiana na Serikali katika kukuza sekta ya Michezo nchini.
"Huwezi kukuza uchumi wa watu bila watu kuwa na Afya njema, ndiyo mana tunadhamini Mabonanza haya kwa lengo la kuwafanya watu wapende kufanya Mazoezi". Amesisitiza
Naye Mwenyekiti wa Bunge Bonanza Festo Sanga,ameipongeza benki ya Azania kwa kukubali kuwa mdhamini wa bonanza hilo kubwa ambalo linalenga kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuhamasisha michezo nchini.
Amesema Magonjwa yasiyo ya kuambukiza yamekuwa mengi nchini na duniani kote ambayo yametokana na watu kuwa na mtindo mbaya wa kula na kutofanya mazoezi.
"Hizi jitihada za Bunge Bonanza ni kuwafanya watu wafanye mazoezi kwa ajili ya kuimarisha Afya zao".
Amesema Azania Bank Bunge Bonanza 2026 limewahusisha Waheshimiwa Wabunge, Watumishi wa Ofisi ya Bunge, Taasisi mbalimbali pamoja na wananchi likiwa na kauli Mbiu usemayo -“UMOJA WETU NI NGUVU YETU.”











Comments
Post a Comment