Mkuu wa Jeshi ya Kujenga Taifa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele ametangaza nafasi kwa vijana kwa ajili ya kushiriki mafunzo ya kujitolea yanayotarajiwa kufanyika Februari mwaka huu.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Tawi la Utawala JKT Brigedia Jenerali Hassan Mabena ambaye amesema utaratibu wa kujiunga na mafunzo hayo ni vijana kuomba na kuchaguliwa katika ofisi za wakuu wa mikoa na wilaya ambao wanawaratibu vijana hao maeneo yao.
”Usaili wa vijana hao kujiunga na mafunzo hayo kwa kujitolea januari 26 mwaka huu katika mikoa yote bara na visiwani kabla ya kuanza kuripoti makambani februari 27 hadi machi 4 mwaka huu,” amesema Brigedia Jenerali Hassan Mabena Mkuu Tawi la Utawala JKT.
Aidha Mabena amesema vijana wenye taaluma kama diploma in information technology, diploma in businessinformation systems na vijana wenye vipaji vya michezo wanahitajika katika mafunzo hayo.
Brigedia Jenerali Mabena pia amesema JKT inawataarifu vijana hao watakaopata fursa hiyo kuwa halitoi ajirawala kuhusika kuwatafutia ajira katika asasi, vyombo vya ulinzi na usalama ama mashieika mbalimbali ya serikali na yasiyo ya serikali.
“sifa za muombaji na maelekezo ya vifaa wanavyotakiwa kwenda navyo ynapatikana katika tovuti ya JKT www.jkt.mil.tz” amesema
Taaria hiyo iliyoandaliwa na mkuu wa JKT Meja Jenerali Mabele imesema vijana hao watajengewa uzalendo, umoja wa kitaifa, ukakamavu, kufundishwa stadi za kazi, stadi za maisha na utayari wa kulijenga na kulitumikia taifa lao.



