Viongozi Waaswa Kuitumikia Jamii

GEORGE MARATO TV
0

Na Ada Ouko, Musoma.

VIONGOZI mbalimbali wa sekta za umma, binafsi , dini wamehimizwa kutumia nafasi waliyonayo kuitumikia jamii huku wakiwa na hofu ya Mungu miyoni mwao.

Mwito huo umetolewa na Msaidizi wa Askofu wa Kanisa Anglikana Dayosisi ya Mara , Manispaa ya Musoma ,Mchungaji David Jason alipokuwa akiongoza ibada ya shukrani ya kumaliza mwaka 2025 na kukaribisha na kuupokea mwaka 2026 katika mkesha wa kuamkia sikukuu ya mwaka huo mpya.


"Tusiende kwa nguvu zetu tukamsahau Mungu, kiongozi mwema ni yule ambaye anaongoza lakini akimtanguliza Mungu kwenye kila shughuli zake, Kwa sababu Mungu pekee ndie anayeweza kutuwezesha kufanya maamuzi sahihi" alisema David.

Alisema katika ibada hiyo ya shukrani kwa kunukuu kupitia biblia Takatifu kitabu cha Joshua 1; 1-9 , na kusema neno la Mungu limewataka waamini wa kikristo kuwa hodari na wajasiri katika kutekeleza shughuli za maendeleo.

"Neno hili lituhase kama jamii ya watanzania ,viongozi wa dini, serikali na viongozi wa sekta ya binafsi kuwa tunapokuwa wajasiri katika kuwaongoza wananchi kwa kutatua changamoto zao tusifanye kwa akili na nguvu zetu tuka msahau Mungu"alisema 







Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top