Hifadhi ya Mikumi yapata hoteli ya kisasa

GEORGE MARATO TV
0


Na Josephat Lazaro 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbas  akiwa na mwenyeji wake Kamishna wa Uhifadhi TANAPA, CPA (T) Musa Nassoro Kuji wametembelea Hifadhi ya Taifa Mikumi kukagua uwekezaji mkubwa wa hoteli iitwayo Mikumi Wildlife Lodge iliyojengwa ndani ya Hifadhi ya Taifa Mikumi.





Uwekezaji huo wa hoteli ya kisasa ndani Hifadhi hiyo ni ishara ya kuwepo kwa mazingira bora ya utalii na uwekezaji nchini ambapo uzinduzi wa hoteli hiyo unatarajiwa kufanyika hivi karibuni utaiweka Tanzania hususani Hifadhi ya Mikumi katika nafasi kubwa ya utalii duniani.

Hoteli ya Mikumi Wildlife Lodge ina zaidi ya vyumba 48 vya kisasa vya malazi vyenye uwezo wa kulaza wageni 96 kwa wakati mmoja, chumba cha mazoezi cha kisasa (gym), sehemu za michezo, ukumbi wa kisasa wa mikutano na mandhari ya kuvutia.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top