MARA
Makamu Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM mzee Steven Masato Wassira ameongoza harambee kubwa ya kuchangia fedha kwa ajili ujenzi na ukarabati ofisi za CCM wilayani Bunda baada ya zilizokuwepo kuteketezwa na moto katika machafuko ya Oktoba 29 mwaka 2025.
Katika harambee hiyo ambayo imeongozwa na mzee Wassira imeshirikisha viongozi mbalimbali wa mkoa wa Mara na kufanyika chuo cha ualimu Bunda ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kuzawali kwa chama hicho.
Akizungumza katika sherehe za maadhimisho ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo February 5,2026, Makamu Mwenyekiti huyo amesema lengo la kujengwa Kwa ofisi ya chama Chama Cha mapinduzi wilaya ya Bunda ni Kwa ajili ya kuskiliza kero za wananchi na kuzitatua.
Kiasi cha shilling Millioni Mia nne arobaini kimechangwa katika harambee hiyo ambapo kiasi kinachotakiwa ili.kumaliza ujenzi wa Ofisi hizo ni shillingi Million mia saba.
"Siwezi kukarabati nyumba yangu wakati wilaya ya bunda haina ofisi ya chama Cha mapinduzi". Amesema
Aidha, Wasira amewataka wanachama wa chama Cha mapinduzi (CCM) kushikamana na kuwa na umoja ili kuwatumikia wananchi.
"Hakuna CCM kama hakuna umoja.na Msingi wa CCM ni umoja".Amesema
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bunda Mayaya Abraham amemshukuru Makamu Mwenyekiti CCM ndugu Wasira pamoja na wana Bunda kwa Michango waliyoitoa kwani kufanya hivyo ni kuunga mkono jitihada za mwenyekiti wa ccm Taifa Rais Samia Suluhu Hassan.
Kwa upande wake mwenyekiti wa ccm mkoa wa Mara Patrick Chandi mbali na kuchangia milioni 12 katika ujenzi huo,amesema ccm mkoa wa Mara ipo imara huku akimpongeza mzee Wassira kwa kukubali kuwa mgeni rasmi wa kutafuta fedha za ujenzi wa jengo hilo la CCM wilaya ya Bunda.
Katika harambee hiyo kada wa CCM na mweka hazina wa CCM wilaya ya Bunda Kambarage Wassira amechangia milioni kumi katika ujenzi wa ofisi hizo za chama.
Naye Mwenyekiti Mstaafu wa CCM mkoa wa Mara Samwel Kiboye amewataka wana Mara kuwa na mshikamano pamoja na kuachana na Makundi Madogo Madogo Kwenye chama.
Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi,pamoja na wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mara yakiingizwa na kauli Mbiu inayosema:𝙏𝙪𝙢𝙚𝙘𝙝𝙖𝙜𝙪𝙖 𝙪𝙢𝙤𝙟𝙖 𝙣𝙖 𝙖𝙢𝙖𝙣𝙞 𝙠𝙬𝙖 𝙢𝙖𝙚𝙣𝙙𝙚𝙡𝙚𝙤 𝙮𝙖 𝙏𝙖𝙞𝙛𝙖 𝙡𝙚𝙩𝙪
Mwiaho























Comments
Post a Comment