Hivi Ndivyo Alivyouawa Mtoto wa Gaddafi

GEORGE MARATO TV
0


 Ripoti ya awali ya uchunguzi kuhusu kuuwawa kwa Saif Al-islam Gaddafi imetolewa mapema leo asubuhi baada uchunguzi uliofanyika kutokana na uchunguzi wa kina wa kitabibu "Autopsy".

Ripoti hiyo imetolewa na kamati ya uchunguzi ya bunge, inaonesha kuwa Idadi ya risasi zilizoingia kwenye mwili wa Saif Al-islam Gaddafi zilikuwa risasi 19, na risasi zilizotolewa mwilini kwake zimeonesha silaha iliyotumika katika mauaji yake ni silaha aina ya Kalashnikov, ni siraha ya kirusi.

Moja ya risasi zilizo mpata ni pamoja na iliyo penya kichwani kwa Saif Al-islam Gaddafi, ambayo ilimpiga juu ya nyusi yake, yani juu ya jicho la kushoto na kutokae kwa nyuma.

Muda ambao mashambulizi ya mauaji yake yaliyo pelekea kifo chake ilikuwa ni saa 05:57 PM saa za Libya.

Kabla nyumba yake kuvamiwa na wauaji kwanza, saa moja na nusu nyuma walinzi wake wote waliondolewa karibu na makazi yake Saif Al-islam, na kubakia yeye pekee yake.

Yani saa moja na nusu kabla ya tukio la uvamizi kutokea walinzi wote waliondolewa kwa sababu zisizojulikana.

Imegundulika kuwa Saif Al-islam Gaddafi alikuwa akitumia namba ya WhatsApp iliyosajiliwa kwa namba za SERBIA, hii ni kulingana na simu yake ambayo baadaye ilipatikana akiwa nayo msaidizi wake anayeitwa Ahmed Al-ajami Al-atiri.

Kwa kawaida Saif Al-islam Gaddafi ana wasaidizi wawili wa kiafrika Hussein Zubeir na Hasheem Al- Zakyt ambao pia akukuwa na wafanyakazi hao wa Kiafrika ndani ya nyumba hiyo wakati wa tukio hilo.

Saa moja na dakika arobaini nyuma kabla ya tukio la kuuwawa kwa Saif Al-islam Gaddafi kutokea Kamera za usalama kuzunguka eneo la makazi yake zote zilizimwa.

Pia kamera za ndani za usalama ambazo zilikuwa zikifanya kazi na zilikuwa zime onganishwa na simu ya mtu mwingine nje ya mji wa Zintan, ambaye anatajwa kuwa karibu la Saif Al-islam Gaddafi imekutwa simu yake haina kumbukumbu yoyote ya tukio la uvamizi na mauaji.

Kwa sehemu kubwa mauaji yake yanaonesha kuwa kuna dalili za Usaliti na uzembe mkubwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top