Jaji Warioba Usiwagawe Watanzania Waunganishe

GEORGE MARATO TV
0


Na David Maphone.

Nimemsikiliza kwa utulivu sana na umakini mkubwa mno Waziri Mkuu mstaafu Mheshimiwa Jaji Joseph Sinde Warrioba kwenye Video clips akihojiwa na Mharri Mkuu wa Gazeti la Jamhuri Tz, Ndugu Jackson M. Manyerere

Kwamba, kwa Kitendo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Jaji Joseph Sinde Warioba mara baada ya mazungumzo yao, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 17 Desemba, 2025.kilijenga matumani makubwa sana

Mara baada ya kutoka taarifa hiyo. mamilioni ya Watanzania walifarijika sana kwa kudhani Kwamba Hekima na Busara za Jaji Warrioba na Mkuu wa nchi Rais Samia Suluhu Hassan kunaweza kuleta mshikamono maelewano ili kuliponya Taifa.

Pamoja na kwamba Mhe, Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba alipewa heshima kubwa ya kuwa kiongozi mkubwa mstaafu wa mwanzo kukutana na kufanya mazungumzo na Rais Samia mara baada ya kuapishwa kuwa Rais Novemba 03, 2025. Katika nyakati Taifa linahitaji uponyaji kutokana na vurugu, Chakusikitisha Mhe, Warrioba kashindwa kuitumia heshima hiyo na kuendeleza uchochezi kipindi tunahitaji Utulivu zaidi ili kujenga mshikamano.

Mzee wangu warioba, kwenye nyakati busara na Hekima zako kuokoa jahazi na dhuruba za kuzama wewe umechagua kulitoboa kabisa tuzama kwanini nasema hivi yapo Maandamano mengine ya nchi mzima yamepangwa tarehe 25/12/2025 wewe umetoka na kauli siku tatu kabla ya Maandamano utaachaje kudhaniwa kwamba

wewe ni mshiriki mwandamizi wa Maandamano hayo?

Mzee wangu warioba umehoji kuwa Polisi, wanajeshi na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama Ndugu zao hajafariki kwenye zile vurugu hapo ulikuwa ukitafuta nini Warrioba kama sio kuchochea ikiwa kama walifiwa na Ndugu zao ili wachukie na kuchukua hatua?

Mzee wangu warioba unasema vyombo vya Ulinzi na Usalama vimegawanyika unautangazia umma kama ni kweli huoni unazidi kuvigawa kwanini ulioopata fursa ya kuongea na Mkuu wa vyomba ya Ulinzi na Usalama Mhe Samia sindio ilikuwa nafasi ya kumshauri na kumsaidi ili kufanikusha kuviunganisha au kwako hilo ni jambo la Sherehe?

Mzee wangu Warioba unasema vifo vya tarehe 29/10/2025 ni vingi Kuliko vifo vya vita Kati ya

Tanzania na Uganda kwa idadi ya kusikia uoni unazidi kuchongamisha Serikali na Wananchi kwa kuwa idadi rasmi haijatolewa kwanini usisubiri ili uje kulinganisha unawahi nini kulisemea hili ?

Mzee wangu warioba kwani unatatizo gani na Serikali?

Mwandishi 

David Maphone

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top