Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana amesema Serikali inalenga kuwa na kampuni zaidi ya laki moja hadi kufikia miaka mitano ijayo ambapo lengo likiwa ni kuongeza idadi kubwa ya wawekezaji vijana pamoja na soko la uzalishaji la ndani ya ili kuepuka kutegemea masoko ya nje.
Akizungumza mapema hii leo Disemba 23, 2025, Waziri Joel Nanauka, katika kikao kazi cha mawaziri kilichoandaliwa na ofisi ya idara ya habari maelezo na kufanyika katika kituo cha urithi wa ukombozi jijini dar es salaam ambapo pia amesema matarajio ya serikali ni kuona zaidi ya ajira milioni moja zinazalishwa.
Aidha, Waziri Nanauka amesema kuwa serikali imebaini kuwa katika idadi kuwa ya vijana waliofanikiwa kupatiwa mikopo wamekosa elimu ya malezi katika uwajibikaji wa biashara mbalimbali kupitia mikopo hiyo, hivyo serikali inalenga kuja na programu ya malezi itakayoweza kuwasaidia vijana kuepukana na changamoto ya kupoteza mitaji yao.
Hata hivyo, Waziri Nanauka ameongeza kuwa serikali imeanza mchakato wa kuanzisha jukwaa la kimtandao la huduma jumuishi litakalosaidia kutoa taarifa mbalimbali pamoja na jukwaa la utoaji wa maoni kwa vijana katika sekta mbalimbali ili kusaidia kuboresha fursa za kiuwekezaji ndani ya nchi.
Sambamba na hilo, Waziri Nanauka amesema kuwa Katika ziara alizozifanya amefanikiwa kubaini mambo muhimu yanayohitqji hatua za haraka ikiwamo ni changamoto ya afya ya akili, ukosefu wa ajira pamoja na matumizi ya dawa za kulevya kwa vijana
Pia, Waziri Nanauka amesema kuwa seriakli itaendelea kuimarisha mazingira wezeshi kwa vijana wabunifu kwa kuendeleza vituo atamizi na vituo vya kulea wabunifu pamoja na kuimarisha mifumo ya ulinzi ya kazi za Sanaa ili kila kijana anufaike kutokana na kazi yake ya Sanaa.
Hata hivyo Katika hatua ya kuimarisha kundi la vijana serikali imepanga kuvifufua vituo vitatu vya maendeleo ya vijana vya Sasanda kilichopo Songwe, Ilonga kilichopo Mororgoro pamoja na Malangu kilichopo Kilimanjaro lengo likiwa ni kuvitumia katika kutoa ujuzi wa vitendo, kujenga uzalendo pamoja na kutoa ustadi wa ujasiliamali na ajira.







