WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Novemba 30, 2025, amekagua Mahakama ya Mwanzo iliyopo Maji ya Chai ambayo iliharibiwa na vurugu zilizotokea Oktoba 29, 2025, mkoani Arusha.
Mheshimiwa Dkt. Mwigulu yupo Arusha kwa ziara ya kukagua mkoa uliojitokeza mjadala wa Oktoba 29, 2025.
Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu ameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Amosi Makalla.




