Edwin Soko asema CCM Yawa Kinara wa Kusikilizwa na Wapiga Kura

GEORGE MARATO TV
0


Mwandishi wa habari  Mwandamizi na mtetezi wa Haki za binadamu Edwin Soko amesema kuelekea kwenye uchaguzi mkuu October 29,2025 , Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeendelea kudhihirisha kuwa ndicho chama kinachosikilizwa zaidi na wapiga kura nchini.

Amesema  hii ni kutokana na misingi yake ya muda mrefu ya uongozi, sera thabiti na mtandao mpana wa kisiasa unaogusa wananchi  kuanzia shina hadi Taifa kwa ujumla  

Akizungumza na waandishi na waandishi wa habari  leo October 28,2025   amefanya uchambuzi wa mwenendo wa kampeni za wagombea wa vyama mbalimbali kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu. 

 "Wananchi waelewe kwamba  takwimu na tafiti mbalimbali za kisiasa zimeonyesha kuwa, licha ya kuwepo kwa vyama vingine vya upinzani vinavyoimarika, CCM bado kinaongoza kwa ushawishi mkubwa katika mijadala ya kisiasa, majukwaani, na hata katika majadiliano ya wananchi mitaani"alisema Soko

Aidha  ameongeza kuwa, Nguvu ya Historia  ni mtaji kwa CCM, chama  kilichoasisiwa mwaka 1977 kufuatia muungano wa TANU na ASP, kimejijengea heshima kupitia historia yake ya kushika hatamu za uongozi kwa zaidi ya miaka 45 hivyo 

Kupitia misingi ya umoja, amani na maendeleo, chama hicho kimeendelea kuwa kinara wa kuaminika kwa Watanzania wengi wanaotafuta uthabiti wa kisiasa na kiuchumi.

Soko amesisitiza kuwa, miongoni mwa sababu zinazoendelea kukifanya CCM kusikilizwa ni pamoja na  viongozi wanaotokana na chama hicho kusimamia utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati, ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), miradi ya nishati kama Bwawa la Julius Nyerere, na kuboresha huduma za afya na elimu.

Baadhi ya wapiga kura waliozungumza na vyombo vya habari wamesema wanakipendelea chama hicho kwa sababu ya uthabiti wake wa kisera na uongozi wa tulivu

Ikumbukwe kua zaidi ya vyama 18 vitashiriki uchaguzi   mkuu kwa mwaka 2025  na wananchi watachagua viongozi watatu akiwemo Raisi wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mbunge pamoja na Diwani

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top