Na Mwandishi wetu Jovina Massano.
MGOMBEA udiwani Kata ya Kamnyonge Jimbo la Musoma mjini mkoani Mara Ladislaus Kutara ameahidi kuboresha miundombinu ya choo na upatikanaji wa huduma bora za kijamii Kata ya Kamnyonge.
Ameyasema hayo wakati akihitimisha kampeni Oktoba 27,2025 na kunadi sera za Chama hicho katika eneo la wazi la Biafra.
Amesema Kata hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi za huduma bora za kijamii ikiwemo afya na Miundombinu ya barabara na ukosefu wa huduma ya choo ofisi ya mtendaji wa Kata hiyo.
"Uboreshaji wa miundombinu ya choo utasaidia upatikanaji wa huduma za mahitaji ya nyumbani karibu kwa wakazi wa Kata hiyo", amesema Ladislaus.
Ameongeza kuwa uwepo wa choo katika ofisi ya mtendaji wa Kata kutapelekea ufanisi kiutendaji.
Kwa Upande wa huduma za Afya amesema ataishauri serikali kuhakikisha upatikanaji wa vifaa tiba hasa madawa ili kuondoa adha ya uhaba wa vifaa tiba kwa wahitaji pindi wanapofika katika Zahanati hiyo.
Aidha ameeleza kuwa atawashauri wakala wa barabara mijini na vijijini TARURA kuweka mitaro katika barabara za Kata hiyo ili kupunguza uharibifu wa barabara na kuwezesha kupitika nyakati zote bila usumbufu.
Uongozi mbovu na kutosimamia miundombinu ya serikali na kuacha ikiharibika na serikali kupoteza mapato ambayo yangeelekezwa kwenye vyanzo vingine vya maendeleo.
Amesema ikiwa Soko la Kata hiyo litaendelea kutofanya kazi ni lazima iangaliwe namna bora na nitaishauri halmashauri ya Manispaa kulibadilishia matumizi liwe soko la nafaka ili wananchi wapate huduma hiyo kwa ukaribu.

