Rai ya Mwandishi wa riwaya za kigiriki Aristophanes

GEORGE MARATO TV
0



Leo katika pita pita zangu nikaamua niwasome waandishi wa kigiriki na nikakutana na Mwandishi mashuhuri  aitwaye *Aristophanes* wa riwaya  🖊️ pendwa mbalimbali .

 *Aristophanes*  alizungumzia  *wajibu wa Vyombo vya Habari katika Taifa Lenye Mgawanyiko wa Kiimani na itikafi.* 

Katika nukuu yake anasema "Vyombo vya habari vina nafasi muhimu katika kujenga na kudumisha umoja wa kitaifa, hususan katika mazingira ambayo taifa linakabiliwa na mgawanyiko wa kisiasa, kijamii au kiitikadi"

 Katika hali kama hiyo, wajibu wa vyombo vya habari  havitakiwi  kuchukua upande mmoja wa mgogoro, bali kuwa daraja linalounganisha pande zinazotofautiana.

Vyombo vya habari vinapaswa kutumia nguvu yake ya mawasiliano kuhimiza mazungumzo ya wazi, kuheshimiana na kueleza kwa umma umuhimu wa umoja, mshikamano na amani ya kudumu. Kupitia taarifa sahihi, usawa wa maoni na uwajibikaji katika kuripoti, vyombo vya habari vinaweza kuwa chachu ya maridhiano na maendeleo ya kitaifa.

Kwa kufanya hivyo, vyombo vya habari vitakuwa vinatimiza jukumu lake la msingi, kuwa sauti ya umma na nguzo ya demokrasia badala ya kuwa chanzo cha migawanyiko au chombo cha upotoshaji wa ukweli.

Nukuu ya Mwandishi huyu inaturudisha darasani kwenye kuzingatia weldi.

Pia inatupa authority role ya kuwaunganisha watu pamoja licha ya kuwa na utofaufi wa  aina yoyote Ile.

Ndugu zangu Wana MISA , sisi tuna wajibu mbele ya taaluma yetu na tuna wajibu mbele ya Taifa letu. Hili ni Taifa la vizazi vyetu, kuanzia kwa babu na bibi zetu, baba na mama zetu , sisi wenyewe na vizazi vyetu vijavyo, tukumbuke tuna wajibu wa kufanya.

 *Edwin Soko* 

 *26.10.2025*

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top