Taasisi ya Mwanamke na Nguvu ya kijani TANZANIA imewaasa wanawake na vijana kuwa makini katika kulinda amani huku ikiwataka kuwa mabalozi wa amani ili kusaidia kujenga kizazi chenye utu na heshima katika jamii .
Hayo yamebainishwa mapema Oktoba 26 mwaka huu 2025, na Mwenyekiti wa Taasisi ya mwanamke na nguvu ya kijani ambaye pia ni Mwenyekiti wa makampuni ya PMM Group Dkt Judith Mhina Spendi katika kongamano la amani la kitaifa lililoandaliwa na taasisi hiyo lenye lengo la kutoa elimu kwa Watanzania kuhusu amani na umuhimu wake katika jamii.
Amesema kuwa Tanzania imejijengea sifa ya kuwa nchi ya amani, utulivu na mshikamano kupitia juhudi mbalimbali zinazoendelea kufanywa na Serikari ikishirikiana na wadau nchini katika kuimarisha hali ya amani.
Hata hivyo Dkt Judith Mhina amewataka watanzania kutotamani nafasi zisizozao katika jamii kwani kufanyq hivyo ni mojo ya sababu ya kuchochea uvunjifu wa amani katika jamii ya watanzania hasa katika kuelekea siku ya uchaguzi oktoba 29.
Aidha Dkt Judith ameipongeza na anaiamini Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kudumisha amani kupitia utawala wake huku akiwatoa hofu watanzania kwani uwepo wa Rais Samia madarakani ni hitajio la mwenyezi Mungu.
Kwa upande wake, Katibu wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) jimbo la kawe, akimwakilisha Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kinondoni, Shaweji Mkumbula, amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi kupiga kura kuchagua viongozi mbalimbali huku akiwatoa hofu juu ya uwepo wa amani katika siku hiyo ya oktoba 29.
Akizungumza kwa niaba ya wajane Bi. Aisha amesema wajane wote hawahitaji migowanyiko wala kufanya vitu vyovyote vyenye viashiria vya uvunjifu wa amani kwa maslahi ya jamii ya watanzania.
Kwa upande wake Mchungaji, Nick Shaboka,akizungumza katika kongamano hilo ambalo limedhaminiwa na kampuni ya PMM GROUP,amesema kuwa muhimili na uti wa mgongo wa taifa ni vijana hivyo inapaswa kuwa makini na huku akiwataka vijana kutokubali kutumika kuchochea vurugu kuelekea siku ya kupiga kura ya oktoba 29 na baada ya tarehe hiyo ya uchaguzi.
Naye Sheikh Abdallah Lugome ameitaka serikali kumchukulia hatua mara moja kwa yeyote anayetishia upotevu wa amani katika jamii kwani kupuuzia vitendo hivyo huweza kuchochea machafuko katika jamii.












