Maafisa Usafirishaji Jimbo ka Mtumba Wahamasika Kushiriki Uchaguzi Oktoba 29.2025

GEORGE MARATO TV
0


Majira ya saa 8 mchana-9 alasiri leo Jumamosi Oktoba 18.2025,waendesha boda boda na bajaji [Maafisa usafirishaji] jimbo la *Mtumba-Dodoma* wapatao *1000* wameungana na Mgombea Ubunge Jimbo la Mtumba *Ndg.Anthony Mavunde*  kuuthibitishia Umma wa Wana Dodoma na Watanzania kwa ujumla kwamba ,wao kama maafisa usafirishaji wako tayari kuitumia haki yao kikatiba kushiriki Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 29 mwaka huu,huku wakimshukuru *Rais Samia* kwa  kuwajengea *Ofisi yao ya Mkoa iliyopo maeneo ya Makole*




Akizungumza nao Mgombea Ubunge kwa tiketi ya *CCM-Jimbo jipya la Mtumba Ndg.Mavunde* amemshukuru Dkt.Samia kwa jitihada madhubuti katika kuiongezea thamani kada hiyo katika sekta binafsi zikiwemo za ujenzi  wa *Ofisi yao ya Mkoa ambayo tayari imekamilika.Ofisi ambayo na yeye pia kama mlezi wa Mkoa wa  Maafisa usafirishaji hao aliwajengea uzio wa ofisi hiyo.*

Aidha amewashukuru kwa namna ambavyo wamekuwa karibu naye wakishirikiana katika kuleta ustawi wa kada hiyo muhimu na kuwaahidi kufanya mambo yafuatayo endapo atachaguliwa kuwa mbunge wa Jimbo jipya la Mtumba.

1:Kuchangia sh.mil 20 katika Mfuko wao wa SACCOS 

2:Kuendelea na ujenzi wa Mabanda Vivuli katika vituo vyote vya pikipiki jimboni kwake

3:Kuwezesha waendesha piki piki kumiliki pikipiki zao wenyewe

4:Kuwezesha kuwepo kwa mazingira rafiki kati yao, Polisi na Migambo wa Jiji 

5:Kushiriki kutatua changamoto ya maegesho kati yao na Wakala wa barabara za mijini na Vijijini[TARURA]

6:Kuwezesha mikopo ya magurudumu[tairi] ya pikipiki kwa kuanzia kulipia sh.elfu 8-10 na kukamilisha malipo kidogo kidogo.








*#MtumbaYenyeKung'araZaidi*

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top