Dkt Nchimbi Atoa Ahadi ya Matumizi Ya Ndege Nyuki 'drones' | Ili Kufukuza Wanyama Waharibifu wa Mazao

GEORGE MARATO TV
0


Mgombea mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania kupitia CCM, Balozi Emmanuel Nchimbi amesema Serikali ijayo ya Chama hicho inakusudia Kutumia ndege nyuki 'Drones' kwa ajili ya kufukuza Wanyama waharibifu katika kata ya Mwaya, Kilombero ili mazao ya wakulima yabaki kuwa Salama.

Dkt Nchimbi ametoa hakikisho hilo leo Oktoba 18, 2025 akiwa katika mkutano wa Kampeni za Urais, ambao umefanyika katika Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro.





Pamoja na mambo mengine ,Dkt.Nchimbi alitumia nafasi hiyo kumuombea kura za ushindi wa kishindo mgombea Urais wa chama hicho,Dkt.Samia Suluhu Hassan pamoja na kumnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Kilombero Ndugu Abubakar Damian ASENGA,pamoja na mgombea Ubunge wa jimbo la Mlimba Ndugu Kellen Rose RWAKATARE  na Madiwani.










Balozi Nchimbi anafikia mkoa wa 25 sasa tangu kuzinduliwa kwa kampeni hizo Agosti 28,2025 jijini Dar es Salaam,akiendelea kusaka kura za ushindi wa kishindo za mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi,Dkt.Samia Suluhu Hassan,Wabunge na Madiwani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top