Bundi atua kwenye kichwa cha Heche na wenzake

GEORGE MARATO TV
0

#Kiza kinene chatanda Chadema



VIONGOZI Wakuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Sasa wanadaiwa kunasa kwenye 'tundu bovu' baada ya kukiuka amri ya mahakama kuu iliyoweka zuio la shughuli za kisiasa kwa Chama hicho.

Tayari viongozi hao akiwemo Makamu Mwenyekiti John Heche na John Mnyika, wameburuzwa mahakamani kwa kosa la kukaidi amri hiyo ya mahakama chini ya Jaji Mwanga.

Kwa mujibu wa shauri jipya lililofunguliwa Mahakama Kuu jijini Dar Es Salaam, imeelezwa kuwa Kina Heche wamenyesha kupuuza amri ya mahakama zaidi ya mara moja.

Shauri Hilo limefunguliwa na Bw. Said ISSA Mohamed.

Kwa mujibu wa hati ya kiapo iliyotolewa na Wakili wa walalamikiwa Mulamuzi Byabusha, licha ya zuio Hilo kati ya MWEZI Juni Hadi Septemba Heche na wenzake walionyesha kukaidi 

Imeelezwa kuwa katika kipindi hicho wadaiwa waliendelea kuitisha na kuandaa mikutano mbalimbali.

Kulingana na hati hiyo ya kiapo kina Heche wanadaiwa kufanywa mikutano ya ndani ikiwemo Ile ya Wandishi wa habari na kutoa maelekezo kadhaa ya kisiasa. Hali inayoonyesha kukaidi na kupuuza Amri Halali ya mahakama hiyo.

Zuio Hilo lilitolewa na Mahakama kuu Juni 10 mwaka huu, kufuatia shauri namba 8960 la mwaka 2025.

Shauri Hilo linalohusu mgawanyo wa Mali za CHADEMA kati ya Bara na visiwani na lilifunguliwa na Bw. Mohamed na wenzake.

Kwa mujibu wa shauri jipya linalomkabili Heche na wenzake, imeelezwa kuwa mbali na amri ya mahakama wadaiwa hao wameonekana kupuuza na kutozingatia.

Kesi hiyo imefunguliwa Mahakama kuu Jijini Dar es salaam Oktoba 2.

Imeelezwa kuwa katika kipindi hicho Cha MWEZI Juni Hadi Septemba Heche, Mnyika na wenzao walikuwa waliendelea kufanya mikutano na kuhamasisha mambo mbalimbali ya kisiasa kinyume na Amri ya mahakama hiyo.

Iwapo madai hayo yatathibitika Heche na wenzake wanaweza kukabiliana na kifungo jela.

Imeelezwa kwamba licha ya amri ya zuio la kufanya siasa, viongozi hao wamekuwa wakiendelea kufanya siasa wazi wazi.

Kulingana na hati hiyo, viongozi hao wamekiuka amri ya mahakama kwa kuhamasisha umma kisiasa na kutoa maagizo mbalimbali.

Hati hiyo ya mashtaka imeiomba mahakama kutoa amri ya kukamatwa kwa Heche na wenzake.

Mbali na Heche na Mnyika, viongozi wengine wanaokabiliwa na tuhuma hizo ni Rose Mayemba na Brenda Rupia.

Wengine ni Hilda Newton, Twaha Mwaipaya na Gervas Bernard Lyenda

Mwisho ..

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top